SEPAH: Israel isijipumbaze kwa nguvu kiduchu za ulinzi wa anga za Marekani
(last modified Thu, 24 Oct 2024 11:55:44 GMT )
Oct 24, 2024 11:55 UTC
  • SEPAH: Israel isijipumbaze kwa nguvu kiduchu za ulinzi wa anga za Marekani

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ameuonya utawala wa Kizayuni "usijitie pepo mpumbavu" na kujidanganya kuwa unaweza kuwa salama kwa nguvu chache za paipu za mifumo ya kujilinda kwa makombora iliyogaiwa na Marekani.

Meja Jenerali Hossein Salami, amesema hayo katika Kongamano la Taifa la Kuwaenzi Mashahidi 9,800 wa Mkoa wa Kermanshah na kusisitiza kuwa, Wazayuni wanapaswa kuelewa vyema kwamba kamwe hawawezi kushinda kwani kadiri watakavyokuwa wamejiandaa kukabiliana na makombora, upande wa pili unavurumisha makombora mengi zaidi na hawawezi kukabiliana nayo.

Vile vile amesema kuwa Israel ni kipande kidogo tu cha ardhi ambacho asilimia 98 ya uchumi wake unatokea usafiri wa baharini. Kadiri unavyokifungia njia za baharini kipande hicho cha ardhi ndivyo unavyozidi kukitia hasara. Uamuzi wowote wa kijinga unaweza kuusambaratisha haraka mno utawala wa Kizayuni. Taifa la Iran liko imara kulinda haki zake na kukabiliana na genge hilo la watu waovu.

Mifumo iliyogaiwa Israel na Marekani haiwezi kuudhaminia usalama utawala wa Kizayuni

 

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH vile vile fikra takatifu ya kufa shahidi katika njia ya Allah ya tangu enzi za vita ya kujihami kutakatifu inaendelea hadi hivi sasa na mifano yake ya wazi inaonekana hivi sasa katika hali nzito wanayoivumilia wananchi wa Ghaza na Lebanon. 

Kamanda Salami ameongeza kuwa katika maeneo hayo ya Ghaza na Lebanon kila siku, asubuhi, mchana na usiku tunashuhudia madhihirisho mapya ya adhama na ukubwa wa imani isiyotetereka ya watu hao. Adui anawavunjia kikatili maeneo yao, anawaulia watoto wao, anaua kwa umati wanawake na vizee lakini Ghaza na Lebanon zimesimama imara kwenye imani thabiti ya Mwenyezi Mungu.