Mashambulizi ya jeshi la Kizayuni dhidi ya Syria
Ndege za kijeshi za utawala wa Kizayuni zimeshambulia kwa mabomu miji ya Damascus na Homs.
Kwa mujibu wa kanali ya Sahab, ikinukuu shirika la habari la IRNA, kufuatia shambulio hilo la mabomu huko Damascus (mji mkuu wa Syria) na Homs, lililofanywa na ndege za kijeshi za utawala wa Kizayuni, mtu mmoja ameuawa na wengine 7 kujeruhiwa.
Katika shambulio hilo, mbali na kushambuliwa eneo la Kafr Sousa, mjini Damascus, moja ya vituo vya kijeshi katika viunga vya Homs (mashariki mwa Syria) pia kimelengwa na jeshi la Kizayuni.
Vile vile jengo moja katika eneo la Kafr Sousa limelengwa na kuharibiwa katika shambulio hilo.
Ulinzi wa anga wa jeshi la Syria umezuia baadhi ya ndege za adui Mzayuni kulenga shabaha zao katika anga za Damascus na Homs.
Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni umekuwa ukishambulia mara kwa mara Damascus na maeneo mengine huko Syria.
Hujuma za kijeshi za utawala wa Kizayuni katika ardhi ya Syria zinatekelezwa katika hali ambayo Damascus imekuwa ikituma barua mara kwa mara kwa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikilaani mashambulizi hayo ya kinyama na kutaka yakomeshwe haraka iwezekanavyo.