Kumbukumbu ya kuuawa shahidi Yahya Sinwar
(last modified Thu, 24 Oct 2024 10:38:33 GMT )
Oct 24, 2024 10:38 UTC
  • Kumbukumbu ya kuuawa shahidi Yahya Sinwar

Karibuni wapendwa wasikilizaji wa Radio Tehran katika Makala yetu ya Wiki ambayo inahusu kumbukumbu ya shahidi Yahya Sinwar aliyekuwa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).

Katika siku kama hizi mwaka mmoja uliopita, Palestina ilifanya oparesheni ya aina yake katika fremu ya mapambano ya ukombozi baada ya kukandamizwa kwa muda wa miaka 75. Kuanzia wakati huo hadi sasa karibu Wapalestina 50,000 wameuawa mbele ya macho ya walimwengu, mamilioni ya wengine wamekuwa wakimbizi, Gaza imebomolewa na kuharibiwa kikamilifu huku picha na filamu zinazoonyesha watu wakichomwa moto wakiwa hai hazijaweza kuamsha dhamiri iliyolala ya mwanadamu. Ismail Haniyeh na wanae wameuawa shahidi, Sayyid Hassan Nasrullah, Fuad Shoukr, Ibrahim Aqil na shakhsia wengine kadhaa wakubwa wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon wote wameuawa shahidi. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshambulia Israel mara mbili na kulenga rasmi vituo na kambi za kijeshi vya utawala wa Tel Aviv. Mifumo wa ulinzi wa makombora ya Israel yaani Kuba la Chuma (Iron Dome) na David's Sling imepoteza hadhi na heshima yake baada ya kutwangwa na Iran. Upande wa kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) watu wamelazimika kuhama nyumba zao, na jeshi la Israel limekwama kwenye mpaka wa Lebanon. Wakati huo huo, Wayemeni kila uchao wamekuwa wakiziwinda ndege za Marekani zisizo na rubani (droni). Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimekata mawasiliano ya baharini kuelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel). Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imezindua kikosi chake cha anga kwa kutekeleza shambulio la ndege isiyo na rubani.

Drone ya Hizbullah

Nani anaamini kuwa haya yote yametokea ndani ya siku 365 tu?! Hebu turudi nyuma kidogo. Wakati Benjamin Netanyahu alipokwenda Oman na kuanzisha rasmi mchakato wa kuanzisha uhusiano baina ya utawala ghasibu na Ulimwengu wa Kiarabu, kwanza alikubaliana na  Sudan, na miezi michache baadaye akawa mkuruba wa Imarati  kwa namna ambayo mahusiano kama hayo hayaonekani kokote isipokuwa katika filamu za Kihindi.  Baada ya hapo ilifuatia Bahrain. Kisiwa hicho kidogo ambacho kinaitegemea kikamilifu Saudi Arabia na misaada yake kwa upande wa uchumi na usalama, kilianzisha uhusiano na Israel, na sasa imefika zamu ya Saudi Arabia. Jitihada za Saudia, nchi ambayo ni kibla cha Ulimwengu wa Kiislamu, za kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel, ulikuwa msumari wa mwisho katika jeneza la Palestina.   

Siku kadhaa nyuma Netanyahu alilalamikia operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa iliyotekelezwa na Hamas wakati alipohutubia katika mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) na kusema: Tulikuwa tumekaribia kufikia mapatano ya kuanzisha uhusiano  kati ya Israel na Saudi Arabia kabla ya operesheni ya Hamas tarehe 7 Oktoba". 

Ghafla, Gaza iliyosahaulika, kuteswa na kukandamizwa liliinuka na kupambana. Wafungwa wa nyumba ya giza ya walikusanya nguvu zao zote na kufanya mapambano dhidi ya maghasibu. Hapa ndipo iliposisika sauti kutoka kwenye kina kirefu cha kisima cha Gaza kwamba bado tuko hai! Kimbunga hicho kililishangaza eneo zima la magharibi mwa Asia.   

Je, unadhani Hamas hawakujua matokeo ya uamuzi wao usiku wa kuamkia Oktoba 7 mwaka jana?! Taarifa yao ipo hadi sasa. Walijua Gaza itabomolewa, walijua kila mmoja wao atalazimika kuwa mkimbizi, walijua kwamba wangelazimika kupigana kwa miezi na labda kwa miaka kadhaa. Walijua hospitali zitachomwa moto, misikiti na makanisa yatateketezwa, walijua kuhusu Wazayuni kutumia mabomu ya za fosforasi, vishada na urani. Walijua Israel itatekeleza mauaji ya kimbari lakini hadi lini? Swali muhimu linaloulizwa ni kwamba kadhia hii inaweza kuendelea hadi lini? Hamas ilijua jibu la swali hili, kwa hiyo ilifanya uamuzi wa mwisho na kuvunjilia mbali mchakato mzima wa kuanzisha uhusiano baina ya utawala ghasibu na nchi za Kiarabu. Hii ndio siri ya ukuu na adhamu ya Oktoba 7 au kile kinachojulikana kama Oparesheni ya Kimbunga cha al Aqsa. 

Vita hivi vinafanana sana na tukio la Ashura lililotokea mwaka wa 61 Hijria. "Haki yote dhidi ya batili yote". Katika vita vya Gaza, kama ilivyokuwa katika uwanja wa Karbala, kunafanyika kila aina ya uhalifu unaoweza kufikirika. Mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza hayakumuacha salama mzee wala mtoto mchanga anayenyonya. Ni ukatili na mauaji yanayofanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya Marekani na nchi za Ulaya, kwa ajili ya kuangamiza kizazi.  

Ni maangamizi ya kizazi ambayo yamelekea kuuawa shahidi Yahya Ibrahim Hassan al Sinwar ambaye amesema: Acheni Karbala nyingine itokee; tunaendeleza  njia yetu ya mapambano." Ni kwa ajili ya kuendeleza njia hiyo ya mapambano ya ukombozi ndipo Ibrahim, mtoto wa Sinwar, akautangazia ulimwengu mzima kwamba: "Kuuawa shahidi baba yangu sio mwisho wa mapambano. Kinachowasubiri Manamrudi katika siku zijazo kitakuwa kibaya sana mara elfu kuliko kile alichoonja Sinwar." 

Yahya Sinwar

Karbala aliyoitengeneza "Yahya" kwa wapigania ukombozi wote duniani inawasubiri "Ibrahim" wapya. Ibrahim ambao watalivunja sanamu kubwa na kuangamiza kabisa utawala wa Manamrudi. Moto wa watawala wenye hulka za Namrud utakuwa "baridi na salama" kwa "akina Ibrahim".  Salamu za Allah ziwe juu ya akina ibrahim na wafuasi wa njia ya Ibrahim, na laana za Mwenyezi Mungu ziwashukie watawala madhalimu, makatili na watenda jinai... sawa kabisa na Namrud (Nimrodi) .....