WFP: Karibu robo ya wananchi wa Somalia wanakabiliwa na njaa kali
Mpango wa Chakula Duniani (WFP) jana ulitahadharisha kuwa karibu robo ya jamii ya watu wa Somalia wanakabiliwa na njaa kali huku watoto zaidi ya milioni 1.85 walio na umri chini ya miaka mitano wakiwa katika hatari ya kupata utapiamlo mkali.
WFP imesema katika taarifa yake kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaweza kupelekea kuongezeka vipindi vya mvua na ukame huko Somalia.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (UNOCHA) pia imeeleza kuwa hali ya ukame imezidi kuwa mbaya katika mikoa ya kaskazini na kuenea hadi katikati na kusini mwa Somalia.
Ofisi hiyo imebainisha kuwa hali ni mbaya hasa katika mikoa ya Nugaal, Mudug, Bari na Sanaag, ambayo inakumbwa na msimu wa nne mfululizo wa mvua kubwa.
"Mamilioni ya watu wako katika hatari ya kuzidiwa na njaa na utapiamlo kutokana na uhaba wa fedha," imeonya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu.
Idadi ya watu watakaopokea msaada wa chakula mwezi huu itapungua hadi 350,000 kutoka watu milioni 1 na laki 1 mwezi Agosti mwaka huu.
Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa UN,bei ya maji imepanda kutoka dola12 hadi 15 kwa pipa la lita 200; na inatarajiwa kupanda zaidi, na hivyo kutatiza maisha ya watu karibu 35,000 waliokimbia makazi katika maeneo mbalimbali katika jimbo la Puntland.
Somalia imestahamili misimu mitano mtawalia ya mvua zilizofeli zilizoiathiri mwishoni mwa 2020 na katika miongo ya hivi karibuni, na kusababisha ukame mkubwa nchini humo mwaka juzi . Hali hiyo ya ukame imesababisha watu milioni 5 kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Mwaka 2011 Somalia ilikumbwa na njaa kali kutokana na ukame na kuuwa watu zaidi ya 26,000.