-
Wasomali wamjia juu Trump baada ya kuwaita "takataka", na kwamba nchi yao "inanuka"
Dec 05, 2025 02:36Matamshi ya dharau yaliyotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu watu na nchi ya Somalia yamesababisha wimbi la hasira na majibu makali.
-
Mbunge Ilhan Omar amjibu Trump kwa kumwita yeye na wahamiaji Wasomali "takataka"
Dec 03, 2025 10:39Ilhan Omar, mbunge Muislamu anayewakilisha jimbo la Minnesota kwa tiketi ya chama cha Democrat amejibu mapigo kwa rais wa nchi hiyo Donald Trump baada ya kiongozi huyo kuanzisha tena mashambulizi ya matusi ya kibaguzi dhidi yake na jamii ya Wasomali wa jimbo la Minnesota.
-
WFP: Karibu robo ya wananchi wa Somalia wanakabiliwa na njaa kali
Nov 21, 2025 03:02Mpango wa Chakula Duniani (WFP) jana ulitahadharisha kuwa karibu robo ya jamii ya watu wa Somalia wanakabiliwa na njaa kali huku watoto zaidi ya milioni 1.85 walio na umri chini ya miaka mitano wakiwa katika hatari ya kupata utapiamlo mkali.
-
Magaidi watatu vinara wa al-Shabaab wauawa katika operesheni ya jeshi la Somalia
Nov 10, 2025 02:20Jeshi la Somalia jana Jumapili lilifanya oparesheni kadhaa katika majimbo ya Bakool na Bay na kuuwa wanachama wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la al Shabaab.
-
Mapitio ya jinai za Magharibi; jinai za Marekani nchini Somalia
Nov 05, 2025 02:36Marekani imefanya mashambulizi ya anga na operesheni za kijeshi nchini Somalia, na kusababisha vifo vingi vya raia, na akthari ya hatua hizo zimekuwa zikikosolewa na makundi ya kutetea haki za binadamu. Idadi halisi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi kuliko ile iliyotangazwa na Pentagon.
-
Somalia yakanusha vikali kufikia makubaliano ya siri na Sweden kuhusu kuwarejesha nchini raia wake
Oct 08, 2025 12:28Ofisi ya Waziri Mkuu wa Somalia leo imetoa taarifa na kukadhibisha vikali Somalia kwamba imefikia makubaliano ya siri na Sweden kuhusu kuwarejesha nyumbani raia wa Somalia kutoka Sweden ukiwemo pia mpango wa msaada wenye masharti kwa Somalia.
-
Wanamgambo washambulia gereza katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu
Oct 05, 2025 07:36Sauti za milipuko na risasi zilisikika pakubwa jana huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia baada ya wanamgambo kushambulia gereza karibu na ikulu ya rais.
-
Somalia yaridhia katiba ya Afrika kuhusu haki na ustawi wa watoto
Oct 02, 2025 07:54Bunge la Shirikisho la Somalia jana lilipasisha Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto baada ya wabunge kukutana mjini Mogadishu.
-
Intelijensia ya Somalia yaua magaidi 24 wa Al Shabaab, yumo kiongozi wake anayewindwa kwa muda mrefu
Sep 27, 2025 02:22Shirika la Intelijensia na Usalama la Somalia (NISA) limetangaza kuwa limetekeleza operesheni ya mashambulizi iliyowalenga viongozi wa kundi la kigaidi la Al-Shabab na kuua magaidi 24 akiwemo kiongozi wa kundi hilo aliyekuwa akisakwa kwa muda mrefu.
-
Rais wa Somalia ataka kusimamishwa vita haraka Ukanda wa Gaza; asikitishwa na masaibu ya Wapalestina
Sep 26, 2025 02:30Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesema kuwa nchi yake inaendelea kutiwa wasiwas sana na mateso na masaibu wanayopitia wananchi wa Palestina na kutaka kufikia mapatano ya kusimamisha vita haraka iwezekanavyo katika Ukanda wa Gaza.