Save the Children: Israel imeua takriban watoto 20,000 huko Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i133412-save_the_children_israel_imeua_takriban_watoto_20_000_huko_gaza
Shirika la Save the Children limesema katika taarifa yake kuwa silaha za kijeshi na mada za milipuko zimeua idadi kubwa zaidi ya watoto duniani kote mwaka 2024, huku Ukanda wa Gaza ukiripoti idadi kubwa zaidi ya vifo.
(last modified 2025-11-21T03:01:11+00:00 )
Nov 21, 2025 03:01 UTC
  • Save the Children: Israel imeua takriban watoto 20,000 huko Gaza

Shirika la Save the Children limesema katika taarifa yake kuwa silaha za kijeshi na mada za milipuko zimeua idadi kubwa zaidi ya watoto duniani kote mwaka 2024, huku Ukanda wa Gaza ukiripoti idadi kubwa zaidi ya vifo.

Shirika la Save the Children limeeleza katika ripoti iliyochapishwa Alhamisi kwamba silaha za milipuko ziliua au kujeruhi watoto wengi mwaka jana kote ulimwenguni. 

Shirika hilo limeeleza kuwa wanajeshi wa Israel wameuwa watu wasiopungua elfu ishirini katika Ukanda wa Gaza tangu Israel ianzisha vita na mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo Oktoba 2023.  

Shirika hilo lisiso la kiserikali limeeleza kuwa kadiri vita vinavyozidi kuhamia katika maeneo ya mjini ndivyo idadi kubwa ya watoto wanavyouliwa. 

Mapema mwakak huu, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) liliripoti kuwa utawala wa Israel unahusika moja kwa moja na vifo au kujeruhiwa watoto zaidi ya 50,000 katika Ukanda wa Gaza. 

Taarifa ya Save the Children imesema: Baada ya Gaza; Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, Sudan, Myanmar, Ukraine, na Syria ndio maeneo ya vita ambayo kumeshuhudiwa vifo vingi zaidi vya watoto mnamo mwaka 2024.

 Huko nyuma,  watoto katika maeneo yenye migogoro na yaliyoathiriwa na vita walikuwa na uwezekano mkubwa wa kufa kutokana na utapiamlo, magonjwa, au mifumo ya afya iliyosambaratika kuliko kutokana na silaha za milipuko. Lakini hii leo, maafisa wa Save  the Children wameeleza kuwa watoto wanalengwa kwa makusudi   katika maeneo mengi ya vita. 

"