Pezeshkian: Iran imeazimia kuimarisha uhusiano na Algeria
(last modified Sat, 02 Nov 2024 03:00:04 GMT )
Nov 02, 2024 03:00 UTC
  • Pezeshkian: Iran imeazimia kuimarisha uhusiano na Algeria

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ameipongeza Algeria kwa kuadhimisha miaka 70 ya mapinduzi yake, akielezea utayarifu wa Iran wa kuimarisha uhusiano na nchi hiyo ya Kiarabu katika nyuga mbali mbali.

Katika ujumbe kwa mwenzake wa Algeria Abdelmadjid Tebboune, Dkt Pezeshkian amepongeza taifa hilo la Afrika kwa kumbukumbu ya  mapinduzi yake ya ukombozi.

Amesema maadhimisho ya miaka 70 ya mapambano ya "ilhamu" ya Algeria ya kupigania uhuru yamefanyika sanjari na kumbukumbu ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Iran na Algeria.

Kadhalika Rais Pezeshkian pia ameeleza utayarifu wa Iran wa kuimarisha na kupanua uhusiano na Algeria katika nyanja mbali mbali. Mnamo Machi 2024, Iran na Algeria zilitia saini hati sita ya ushirikiano wakati wa ziara rasmi ya rais wa zamani wa Iran, Ebrahim Raisi huko Algiers.

Makubaliano hayo yanahusu kukuza ushirikiano katika sekta ya mafuta na gesi, sayansi na teknolojia, uchumi unaotegemea maarifa, sekta ya utalii, michezo na sekta ya habari.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa, umoja na mshikamano ni miongoni mwa mahitaji muhimu zaidi ya ulimwengu wa Kiislamu hii leo na kwamba, umoja huo ndio dawa mjarabu ya kukabiliana na njama, fitina na chokochoko za maadui wa Waislamu.

Tags