Velayati: Haikufikiriwa kama Uturujki ingenasa katika mtego wa Marekani na Wazayuni
Dr. Ali Akbar Velayati, mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya iran katika masuuala ya kimataifa ameashiria machafuko ya hivi karibuni ya magaidi nchini Syria na kusema: "Kwa bahati mbaya Uturuki imekuwa chombo katika mikono ya Marekani na utawala wa Kizayuni."
Velayati amebainisha kwamba, haikufikiriwa kuwa Uturuki pamoja na historia yake ya Kiislamu, ingeangukia katika mtego wa Marekani na Wazayuni.
Akizungumzia nafasi ya Uturuki katika machafuko ya hivi karibuni nchini Syria, mshauri wa kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema: Watu wa Uturuki ni Waislamu watiifu, wasio na misimamo mikali na miongoni mwa mataifa ambayo yametoa huduma kubwa Uislamu na hesabu yao ni kando ikilinganishwa na wengine.
Dr. Velayati aliongeza: "Tulikuwa na matumaini kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, ambaye ni mtu mwenye uzoefu katika nyanja ya kiiintelijensia na sera za kigeni, angetatua matatizo hayo."
Velayati ameyachukulia mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa hivi karibuni dhidi ya Syria kuwa ni hatua iliyopangwa kabla ya waendesha vyombo vya habari vya Magharibi na madola ya kimataifa na akasema: Wanapotosha ukweli wa mambo, kwa sababu kabla ya hapo walijifanya kuwa na maoni ya umma ya nchi za Magharibi kwamba utawala wa Kizayuni umeshinda vita vya Lebanon na Sasa wanadai kwamba kundi la kigaidi la "Tahrir al-Sham" nchini Syria hivi karibuni litapindua serikali halali ya Bashar al-Assad.