Mamilioni wauswalia mwili wa Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mjini Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139652-mamilioni_wauswalia_mwili_wa_kiongozi_shahidi_ayatullah_sayyid_ali_khamenei_mjini_tehran
Mamilioni ua waombolezaji wameshikiri Swala ya maiti ya mwili mtakatifu wa Imam shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na kundi la wanafamilia wake watukufu iliyofanyika kwa uwepo mkubwa wa viongozi wa serikali, jeshi na umma kwa ujumla.
(last modified 2026-07-05T07:21:25+00:00 )
Jul 05, 2026 07:15 UTC
  • Mamilioni wauswalia mwili wa Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mjini Tehran
    Mamilioni wauswalia mwili wa Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei mjini Tehran

Mamilioni ua waombolezaji wameshikiri Swala ya maiti ya mwili mtakatifu wa Imam shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na kundi la wanafamilia wake watukufu iliyofanyika kwa uwepo mkubwa wa viongozi wa serikali, jeshi na umma kwa ujumla.

Swala hiyo iliongozwa na Marja’a wa Kidini, Ayatullah Ja’far Subhani, katika hali ya huzuni na uaminifu wa hali ya juu, huku ikihudhuriwa na umati mkubwa uliodhihirisha ukubwa wa ushiriki wa watu katika hafla ya kuaga.

Tangu mapema kabisa alfajiri, mafuriko ya watu kutoka Tehran na mikoa mbalimbali ya nchi walijitokeza katika Musalla wa Imam Khomeini (Mungu amrehemu) ili kushiriki katika ibada hii ya kiroho na kumuaga kiongozi aliyeuawa shahidi wa mapinduzi pamoja na familia yake.

Eneo la Musalla lilijaa kwa kusomwa aya za Qur’an Tukufu, maombolezo na tenzi za huzuni, huku waliohudhuria wakimswalia Mtume (saw) na kusoma Suratul-Fatiha kwa ajili ya kuwaenzi mashahidi hao.

Baada ya kuswaliwa swala ya maiti, miili mitakatifu ya kiongozi aliyeuawa shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na wanafamilia wake ilibebwa juu ya mabega ya waombolezaji ili kuendelea na marasimu ya mazishi.

Shughuli za mazishi zitaendelea leo na kesho jijini Tehran. Ratiba nyingine imepangwa katika mji mtakatifu wa Qom, ikifuatiwa na kisha katika miji ya Karbala na Najaf nchini Iraq, kabla ya maziko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran tarehe 9 Julai.