Maonyesho ya bidhaa za Maabara yafunguliwa Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i120096-maonyesho_ya_bidhaa_za_maabara_yafunguliwa_tehran
Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya Vifaa vya Maabara Vilivyotengenezwa nchini Iran yaliyopewa jina la 'IRAN LAB EXPO' yamefunguliwa leo Tehran.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Dec 13, 2024 06:33 UTC
  • Maonyesho ya bidhaa za Maabara yafunguliwa Tehran

Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya Vifaa vya Maabara Vilivyotengenezwa nchini Iran yaliyopewa jina la 'IRAN LAB EXPO' yamefunguliwa leo Tehran.

Maonyesho hayo ambayo yataendelea hadi tarehe 16 Disemba, yamefunguliwa na Dk Hossein Afshin, Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia masuala ya Sayansi na Teknolojia, Dk Hossein Simaei Sarraf, Waziri wa Sayansi pamoja na maofisa wengine wa ngazi za juu katika sekta hiyo. Maonyesho hayo yanafanyika sambamba na Maonyesho ya 25 ya Mafanikio ya Utafiti, Teknolojia na Soko la Teknolojia.

Bidhaa zaidi ya 10,000 za ubunifu ambazo zimeundwa nchini Iran zinaonyesha katika maonyesho hayo yanayofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Maonyesho cha Tehran.

Jumla ya kampuni 278 zenye msingi wa maarifa ya kisayansi, Knowledge Based, zinawasilisha mafanikio yao ya hivi karibuni, na vifaa vya maabara na upimaji wa wa kisasa. Maonyesho hayo yanalenga zaidi kupanua soko la ndani na la kimataifa kwa kampuni.

Maonyesho hayo ya 12 yanaonyesha bidhaa zilizotengenezwa na Iran katika nyanja tofauti zikiwemo 'Mafuta, Gesi na Petrokemikali, 'Umeme na Vfaa vya Umeme', ', Program za Kompyuta, 'Mekaniki', 'Kemia na Metallurgy', 'Kilimo na Mazingira ', ' Fizikia ya Msingi', 'Vifaa vya Maabara ya Jumla', 'Vifaa na Mashine katika Teknolojia za Mkakati, ‘Uhandisi wa Tiba na Vifaa vya Biolojia and Biomaterials’, ‘Vifaa vya Maabara, ‘Vifaa Vya Elimu, ‘Maabada ya Viwanda, na ‘Huduma za Ujenzi.

Maonyesho hayo pia yanatumika kama jukwaa la kampuni husika kufanya mikutano ya kibiashara, kubadilishana maarifa, kuunda fursa za biashara na kufahamiana na uwezo wa kampuni zingine, na vilevile masoko yanayoweza kutokea.

Asilimia 90 ya vifaa vya matibabu vinavyotumiwa hospitalini nchini Iran vinatengenezwa nchini na vilivyosalia vinaagizwa kutoka nchi ya nchi.

Iran inashikilia nafasi ya kwanza katika Asia Magharibi kwa kutengeneza vifaa vya matibabu  ambapo kwa sasa bidhaa zenye thamani ya karibu dola milioni 50 zinauzwa katika nchi 40 kila mwaka.