Kiwango cha safari za meli za kibiashara za Iran kimeongezeka sana
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i120154-kiwango_cha_safari_za_meli_za_kibiashara_za_iran_kimeongezeka_sana
Ali Akbar Safaei, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bandari na Safari za Baharini la Iran amesema kuwa: Uwezo wa meli za kibiashara za Jamhuri ya Kiislamu umeongezeka sana na kufikia meli 87 baada ya wataalamu wake wa ndani kutengeneza meli mpya zaidi na nyingine kununua kutoka nje.
(last modified 2024-12-14T23:37:31+00:00 )
Dec 14, 2024 23:37 UTC
  • Kiwango cha safari za meli za kibiashara za Iran kimeongezeka sana

Ali Akbar Safaei, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bandari na Safari za Baharini la Iran amesema kuwa: Uwezo wa meli za kibiashara za Jamhuri ya Kiislamu umeongezeka sana na kufikia meli 87 baada ya wataalamu wake wa ndani kutengeneza meli mpya zaidi na nyingine kununua kutoka nje.

Vilevile amesema kuwa, bandari na vifaa vya baharini vimeboreshwa na kustawishwa zaidi nchini Iran na hayo ni mafanikio mengine ya shirika lake katika kutia nguvu uwezo wa biashara za baharini wa Jamhuri ya Kiislamu.

Amesema: "Licha ya kwamba Iran iko chini ya vikwazo vya kikatili, lakini imeweza kwa kutumia uwezo na nguvu zake za ndani, kujiimarisha zaidi katika safari za baharini. Aidha amesema, hivi sasa zaidi ya asilimia 80 ya vifaa vya baharini na bandari za Iran ziko katika ubora wa hali ya juu na zinafanya kazi kubwa kila siku.

Naye Jalil Eslami, Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Bandari na ya Kiuchumi katika Shirika la Bandari la Iran amesema kwamba, kuna ongezeko la wastani wa asilimia 15 katika utendaji wa bandari za kibiashara za Iran hivi sasa.

Ameongeza kuwa: Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Iran imekuwa na ustawi wa kutosha wa ubora wa bandari na vifaa vya baharini, katika masuala ya uokoaji na utoaji huduma, masuala ya mabaharia, utoaji vibali vya baharini pamoja na kulinda usalama na ulinzi wa mazingira ya baharini.