Marekani na Ujerumani, washirika wa mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i120316-marekani_na_ujerumani_washirika_wa_mauaji_ya_kimbari_yanayofanywa_na_wazayuni_gaza
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameashiria sehemu ya maelezo yaliyotolewa na Ben Saul, ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa, kwamba Ujerumani na Marekani zinachangia asilimia 99 ya silaha inazopatiwa Israel na akabainisha kwamba nchi hizo mbili ni washirika wa mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2024-12-18T23:38:19+00:00 )
Dec 18, 2024 23:38 UTC
  • Marekani na Ujerumani, washirika wa mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni Gaza

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameashiria sehemu ya maelezo yaliyotolewa na Ben Saul, ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa, kwamba Ujerumani na Marekani zinachangia asilimia 99 ya silaha inazopatiwa Israel na akabainisha kwamba nchi hizo mbili ni washirika wa mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Esmaeil Baqhaei, amesema, Marekani na Ujerumani zinasaidia na kushiriki katika mauaji ya kimbari huko Gaza kwa kuendelea kuupelekea silaha utawala wa Kizayuni wa Israel na kwa hivyo nchi hizo mbili zimekuwa washirika kamili wa mauaji hayo.

Bila shaka, inapasa izingatiwe pia kuwa, Marekani na Ujerumani si washirika wa mauaji ya kimbari ya Gaza pekee, lakini zimefanya pia jinai zisizohesabika katika nchi nyingine ikiwa ni pamoja na Afghanistan na Iraq; na ushirikiano zinaotoa Marekani na Ujerumani kwa Israel katika mauaji ya kimbari ya Gaza umeanika na kuweka tena hadharani uovu na jinai zao.

Kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa ya Stockholm (SIPRI) na kutolewa ripoti yake mwezi Machi, Marekani na Ujerumani zinachangia karibu asilimia 99 ya silaha zote zinazoagizwa na utawala ghasibu wa Israel. Kwa mujibu wa makadirio yaliyofanywa na SIPRI, utawala wa Kizayuni umeagiza asilimia 69 ya silaha zake kutoka Marekani na asilimia 30 kutoka Ujerumani katika kipindi cha mwaka 2019-2023.

 

Halo katika mtaa mmoja ulioshambuliwa na Israel huko Gaza kwa kutumia silaha za Marekani na Ujerumani

Wakati walimwengu wanataka usitishwe mwenendo wa kuipelekea silaha utawala haramu wa Israel, Marekani na Ujerumani zinaendelea kuupatia silaha utawala huo ghasibu, jambo ambalo, si tu linaonyesha zinavyodharau miito ya walimwengu, lakini pia limeonyesha kuwa, kulinda uwepo wa utawala wa kibaguzi wa Kizayuni ni muhimu zaidi kwa Magharibi kuliko kuzuia mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa Gaza.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa, zaidi ya Wapalestina 45,000 wameuawa shahidi tokea Oktoba mwaka jana, katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na aghalabu ya waliouawa ni wanawake na watoto huku wengine zaidi ya laki moja elfu tano wakiwa wamejeruhiwa. 

Wakati Muqawama na mapambano ya watu wa Gaza ya kukabiliana na mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel yalikuwa yameufanya utawala huo uwe katika hatari ya kushindwa kikamilifu, misaada ya kila upande kutoka Magharibi hasa Marekani na Ujerumani ndiyo iliyouwezesha utawala huo kuendeleza mashambulizi na jinai zake katika Ukanda wa Gaza.

 

Baadhi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza kwa himaya ya nchi za Magharibi hasa Marekani na Ujerumani

Kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, madola ya Magharibi yanakiuka kanuni za kisheria za msingi wa "kuheshimu na kutoa hakikisho la kuchunga" sheria za masuala ya kibinadamu, pamoja na wajibu wao wa kisheria wa kimataifa kuhusu uzuiaji na utoaji adhabu kwa ufanyaji mauaji ya kimbari. Kwa msingi huo Marekani na Ujerumani inapasa zibebeshwe dhima na ziwajibishwe kutokana na vitendo vya kihalifu na kijinai zinavyofanya.    

 Kile kinachotokea sasa hivi katika Ukanda wa Gaza ni kuwakomoa kwa visasi watu madhulumu kupitia mbinu na njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya mauaji ya kimbari, kuwatesa kwa njaa na kuwaandama kwa mashambulio ya kinyama; ambapo yote hayo hayawezi kuendelezwa na Israel bila msaada wa Marekani na nchi za Ulaya hasa Ujerumani.