Jeshi la IRGC la Iran laanza mazoezi makubwa kuimarisha utayari wa kivita
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121012-jeshi_la_irgc_la_iran_laanza_mazoezi_makubwa_kuimarisha_utayari_wa_kivita
Kikosi cha nchi kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limeanzisha mazoezi makubwa na maalum katika jimbo la Kermanshah magharibi mwa Iran, kama sehemu ya juhudi za kuongeza utayari wao wa kivita na kujiandaa zaidi kukabiliana na vitisho vya usalama dhidi ya nchi.
(last modified 2025-01-04T10:05:51+00:00 )
Jan 04, 2025 10:05 UTC
  • Jeshi la IRGC la Iran laanza mazoezi makubwa kuimarisha utayari wa kivita

Kikosi cha nchi kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limeanzisha mazoezi makubwa na maalum katika jimbo la Kermanshah magharibi mwa Iran, kama sehemu ya juhudi za kuongeza utayari wao wa kivita na kujiandaa zaidi kukabiliana na vitisho vya usalama dhidi ya nchi.

Mazoezi hayo, yenye jina la Payambar-e-A'adham (Mtume Adhimu) 19, yalianza katika eneo la vita magharibi mwa Iran Jumamosi, yakishirikisha sehemu mbalimbali maalum na vitengo vya Kikosi cha Nchi Kavu cha IRGC, hasa kutoka Brigedi za Mirza Kuchak Khan.

Katika hatua ya kwanza ya mazoezi ya vita, hali tofauti za operesheni za majibu ya haraka zilifanyiwa mazoezi.

Uhamishaji wa haraka wa askari na vifaa vya kijeshi kwenye eneo la mazoezi ulifanyika katika sehemu ya kwanza ya mazoezi hayo.

Vikosi vya kijeshi vya Iran hufanya mazoezi ya mara kwa mara kulingana na ratiba ya kina katika sehemu mbalimbali za nchi ili kujaribu silaha zao na vifaa na kutathmini utayari wao wa kivita.

Maafisa wa nchi Iran wamesisitiza mara kwa mara kwamba nchi haitasita kuimarisha uwezo wake wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na nguvu zake za makombora, ambazo zinalenga kabisa kujihami, na kwamba uwezo wa ulinzi wa Iran hautawahi kuwa sehemu ya mazungumzo.