Araghchi: Muqawama unaimarika licha ya kuwepo njama za maadui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121150-araghchi_muqawama_unaimarika_licha_ya_kuwepo_njama_za_maadui
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema fikra za muqawama zimekuwa zikiimarika katika miezi ya hivi karibuni licha ya majaribio ya maadui ya kudhoofisha fikra hizo.
(last modified 2025-01-07T23:17:37+00:00 )
Jan 07, 2025 23:17 UTC
  • Araghchi: Muqawama unaimarika licha ya kuwepo njama za maadui

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema fikra za muqawama zimekuwa zikiimarika katika miezi ya hivi karibuni licha ya majaribio ya maadui ya kudhoofisha fikra hizo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kumuenzi kamanda wa kupambana na ugaidi aliyeuawa wa Iran Jenerali Qassem Soleimani Jumanne, Araghchi amesema maadui hawatambui ukweli kwamba damu ya mashahidi ni silaha mikononi mwa muqawama.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Iran alimsifu zaidi Shahidi Jenerali Soleimani kwa kuimarisha muqawama kiutendaji na kuufanya kuwa harakati inayosimama imara katika eneo la Asia Magharibi na kupambana na Israel na satwa ya kibeberu ya Magharibi.

Jenerali Soleimani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), aliuawa Januari 3, 2020 pamoja na wenzake katika shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za Marekani lililoidhinishwa na Rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.

Alikuwa anaheshimiwa sana katika Asia ya Magharibi kwa jukumu muhimu alilotekeleza la kupambana na kundi la kigaidi la Daesh Takfiri nchini Iraq na Syria.

Pia katika hotuba yake, Araghchi aliashiria mauaji ya viongozi wa muqawama, akiwemo Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah, yaliyofanywa na Israel.

Alisema: "Sina shaka kwamba damu ya Shahidi Nasrallah itaifanya Hizullah kuwa na nguvu na weledi zaidi."

Akigusia matukio ya hivi karibuni nchini Syria, alisema jeshi la Syria lilipata pigo la kisaikolojia kabla ya pigo la kijeshi kupitia vita vya vyombo vya habari, akibainisha, "Jeshi la Syria lilishindwa kabla ya kupambana, na lilishindwa kupigana."