Mwanadiplomasia wa zamani wa Iran: Mazungumzo na Marekani yanaendelea vizuri
Msemaji wa zamani wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran na balozi wa zamani wa Iran nchini Italia amesema: "Mazungumzo na Marekani yamekuwa na mwanzo mzuri kimuundo na kiujuma.
Sayyid Muhammad Ali Husseini amesema, makubaliano kati ya pande husika ya kuzingatia mazungumzo ya kuondoa vikwazo na suala la nyuklia, na mchakato wa mazungumzo na Marekani unaendelea vizuri."
Duru ya kwanza ya mazungumzo hayo ilifanyika Jumamosi iliyopita Aprili 12 nchini Oman.
Katika duru ya kwanza ya mazungumzo, pande mbili zilikubaliana kwamba msingi wa mazungumzo hayo utakuwa ni "Iran kufanya iaminike na itoe hakikisho kwamba programu yake ya nyuklia ni ya malengo ya amani" na mkabala wake "iondolewe vikwazo na Marekani kwa namna itakayokuwa na taathira"
Mwanadiplomasia huyo wa Iran amesema, kwa kuzingatia uzoefu wa thamani wa timu ya mazungumzo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kujitolea kwao katika juhudi za makusudi na makini za kupata maslahi ya kitaifa ya Iran, tuna imani kwamba timu yetu haitapiga hatua moja mbele hadi ihakikishe mkondo sahihi na mchakato sahihi wa mazungumzo hayo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi ameashiria kumalizika kwa duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana ya nyuklia kati ya Iran na Marekani yaliyofanyika jana Jumamosi mjini Rome, Italia na kueleza kwamba, mazungumzo ya kiufundi katika ngazi ya wataalamu yataanza siku ya Jumatano nchini Oman.