Msemaji wa Wizara ya Ulinzi: Hakukuwa na shehena za zana za kijeshi katika Bandari ya Shahid Rajaee
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa uchunguzi unaonyesha kuwa hakukuwa na shehena iliyoingizwa nchini au kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya fueli au kwa matumizi ya kijeshi katika eneo la tukio la moto katika Bandari ya Shahidi Rajaee.
Akizungumzia habari na uvumi kuhusu tukio la Bandari ya Shahidi Rajaee, Brigedia Jenerali Reza Talaei-Nik amesema: "Kwa mujibu wa uchunguzi na nyaraka, hapakuwa na mizigo iliyoingizwa au iliyosafirishwa nje kwa ajili ya fueli au matumizi ya kijeshi katika eneo la tukio la moto katika Bandari ya Shahidi Rajaee, na baadhi ya habari zinazosambazwa kwa makusudi na vyombo vya habari vya kigeni kwa ajili ya kuunga mkono vita vya kisaikilojia vya adui, sio jambo geni, na zimekuwa zikizimwa kutokana na kuwa macho na makini kwa taifa la Iran.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Iran ameongeza kuwa: "Kama ilivyoripotiwa, sababu za tukio la moto la Bandari ya Shahidi Rajaee, iwe sababu za usalama au kiusalama zitatangazwa na maafisa husika kwa wakati unaofaa."
Talaei Nik amesisitiza kuwa: Hakukuwa na shehena iliyoingizwa au kusafirishwa nje kwa ajili ya fueli au matumizi ya kijeshi katika eneo la tukio na katika Bandari ya Shahidi Rajaee kwa ujumla.
Hadi jana, watu 28 waliripotiwa kuaga dunia na mamia ya wengine wamejeruhiwa katika mlipuko mkubwa uliotokea kwenye Bandari ya Shahid Rajaee yenye eneo la hekta zipatazo 2,400, katika mji wa Bandar Abbas, kusini mwa Iran.