Araghchi kufanya safari Saudi Arabia na Qatar kwa shughuli za kidiplomasia
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anatazamiwa kuzuru Saudi Arabia na Qatar Jumamosi ya kesho ikiwa ni sehemuu ya juhudi mpya za kuimarisha uhusiano na majirani wa eneo hili.
Hayo ni kwa mujibu wa Ismail Baghaei, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Esmaeil Baghaei aliwaambia waandishi wa habari kuwa "Kwa mujibu wa sera ya msingi ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuimarisha uhusiano mara kwa mara na majirani, Waziri wa Mambo ya Nje atasafiri kwenda Riyadh siku ya Jumamosi kukutana na maafisa wakuu wa Saudia."
Aliongeza kuwa Araghchi ataelekea Doha baadaye siku hiyo ili kushiriki katika mkutano wa kilele wa Mazungumzo ya ulimwenguu wa Kiarabu na Iran.
Ziara hizo zinakuja huku kukiwa na matukio ya mienendo ya kikanda na mkakati unaoendelea wa Tehran wa kujenga upya uaminifu na ushirikiano na mataifa ya Ghuba ya Uajemi. Huku mivutano ikibadilika katika eneo la Asia Magharibi, diplomasia ya moja kwa moja na Saudi Arabia na kushiriki katika Mazungumzo ya Kiarabu yanaashiria hatua muhimu katika sera ya ujirani-kwanza ya Iran.
Iran imekuwa ikifanya kazi ya kurejesha uhusiano wake katika Ghuba ya Uajemi, hususan baada ya mvutano wa miaka ya hivi karibuni wa kidiplomasia na Saudi Arabia. Safari ya kwenda Doha kwa ajili ya mkutano wa Mazungumzo ya Iran na Nchi za Kiarabu inaonyesha lengo pana la Tehran la kujiweka kama sauti kuu katika kuunda mazungumzo na usalama wa kikanda.