'Khorramshahr-5' kuwa kombora la kwanza la balestiki la Iran linalovuka mabara?
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128856
Tetesi zinazoongezeka kuhusu Khorramshahr-5, kombora la kwanza la Iran linaloweza kuvuka mabara (ICBM), zinaonyesha kwamba hivi karibuni nchi hii inaweza kujiunga na kundi dogo la nchi zenye silaha za aina hiyo.
(last modified 2025-07-28T08:32:30+00:00 )
Jul 28, 2025 07:23 UTC
  • 'Khorramshahr-5' kuwa kombora la kwanza la balestiki la Iran linalovuka mabara?

Tetesi zinazoongezeka kuhusu Khorramshahr-5, kombora la kwanza la Iran linaloweza kuvuka mabara (ICBM), zinaonyesha kwamba hivi karibuni nchi hii inaweza kujiunga na kundi dogo la nchi zenye silaha za aina hiyo.

Katika siku za hivi karibuni, ripoti zimekuwa zikitolewa kuhusu kombora la Khorramshahr-5, ICBM, lenye uwezo mkubwa sana. Linaripotiwa kuwa na uwezo wa kupiga umbali wa kilomita 12,000, kasi ya Mach 16, na kichwa chenye uzito wa tani 2.

Tofauti na hapo awali ambapo habari za mafanikio makubwa ya kijeshi ya Iran zimekuwa zikitangazwa na Wizara ya Ulinzi au Kikosi cha Wanaanga wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), habari za Khoramshahr-5 zimetoka kwa vyanzo visivyo rasmi.

Baadhi ya vyombo vya habari vimetoa ripoti ambayo si za kweli kwamba kombora hilo tayarii limefanyiwa majaribio, lakini vimeonyesha picha za jaribio la Khorramshahr-4 hapo 2023. Hata hivyo, uwezekano kwamba kombora hilo liko tayari hauwezi kukanushwa.

Viongozi wa Iran, wakiwemo wale wa IRGC, siku za nyuma walikanusha kutengeneza kombora la kuvuka mabara, ICBM, wakisema kuwa makombora yaliyopo sasa hapa nchini yanatosha kuzima vitisho vya utawala wa kizayuni wa Israel na vituo vya Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia.

Hata hivyo, kufuatia matukio ya hivi karibuni na uchokozi wa Israel na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, kuna uwezekano kwamba msimamo huo wa muda mrefu unaweza kubadilishwa.

Kasi ya kombora Khorramshahr-5 imeripotiwa kuwa Mach 16, takriban kilomita 20,000 kwa saa.