Zarif na Cavusoglu wajadili masuala ya kieneo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i13585-zarif_na_cavusoglu_wajadili_masuala_ya_kieneo
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Mevlut Cavusoglu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amekutana na kufanya mazungumzo hapa Tehran na Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwa muda wa masaa matano.
(last modified 2026-02-22T02:21:18+00:00 )
Aug 19, 2016 16:43 UTC
  • Zarif na Cavusoglu wajadili masuala ya kieneo

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Mevlut Cavusoglu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amekutana na kufanya mazungumzo hapa Tehran na Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwa muda wa masaa matano.

Bahram Qassimi ameeleza kuwa Mevlut Cavusoglu jana alifanya safari fupi hapa Tehran kwa lengo la kufuatilia makubaliano na mashauriano yaliyofanyika kati ya maafisa wa nchi mbili hizo katika ziara ya wiki iliyopita ya Muhammad Javad Zarif huko Ankara, Uturuki. Katika mazungumzo hayo, mawaziri hao wawili wamebadilishana mawazo kuhusu matukio ya kieneo na uhusiano wa pande mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran (kushoto), akiwa na waziri mwenzake wa Uturuki

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa, Tehran na Ankara zilikubaliana kwamba viongozi wa nchi mbili wawe wakikutana na kufanya mazungumzo ya mara kwa mara na kwamba mazungumzo hayo yafanyike katika ngazi mbalimbali. Pande mbili hizo zilikubaliana kutekeleza hayo kufuatia ziara ya wiki iliyopita ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mjini Ankara na mazungumzo yake ya masaa kadhaa na Rais wa nchi hiyo na maafisa wengine wa ngazi ya juu wa Uturuki.