Ayatullah Amoli Larijani: Istiqama ya taifa imeshinda 'kiburi kibaya cha US-Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139176-ayatullah_amoli_larijani_istiqama_ya_taifa_imeshinda_'kiburi_kibaya_cha_us_israel
Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesifu istiqama na ushujaa wa taifa kubwa la Iran mbele ya "kiburi kibaya" cha Marekani na utawala wa Israel.
(last modified 2026-06-16T03:01:58+00:00 )
Jun 16, 2026 02:59 UTC
  • Ayatullah Amoli Larijani
    Ayatullah Amoli Larijani

Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesifu istiqama na ushujaa wa taifa kubwa la Iran mbele ya "kiburi kibaya" cha Marekani na utawala wa Israel.

"Damu safi ya mashahidi fahari wa vita vya kikatili, hasa damu safi ya kiongozi wetu mpendwa na mtukufu, Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ilikuwa pumzi tukufu mbayo hatimaye imeibua harakati na mwamko wa taifa zima,"ameandika Ayatullah Amoli Larijani katika akaunti yake ya X baada ya kufikiwa makubaliano kati ya Tehran na Washington.

Ameongeza kuwa:" Uzoefu huu kwa mara nyingine tena umedhihirisha ukweli kwamba ngome ya Iran ya Kiislamu inahifadhiwa tu kutokana na ushiriki wa wananchi, mapambano ya vikosi vya ulinzi na juhudi za mamlaka za mfumo wa Kiislamu.

Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, anaona kuwa ni wajibu wake kutoa heshima za dhati na pongezi kwa mapambano haya makubwa, na anamuomba Mwenyezi Mungu ayajalie istiqama na uchamungu matabaka yote ya jamii, wanajeshi weledi wa majeshi ya ulinzi na maafisa wa nchi.

Siku ya Jumapili, Sekretarieti ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran lilitangaza kuwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Tehran na Washington mapema siku hiyo yatahitimisha vita katika pande zote, ikiwa ni pamoja na nchini Lebanon. Zaidi ya hayo, mzingiro wa majini dhidi ya Iran pia utakomeshwa kikamilifu mara moja.

Sekretarieti ya SNSC ilisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, chini ya mwongozo wa Kiongozi wake shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kwa maelekezo ya Kiongozi wa sasa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, kwa uungwaji mkono thabiti wa wananchi wa Iran, na kwa juhudi zisizokoma za vikosi vya ulinzi vya nchi hii, imefanikiwa kukamilisha kipindi kigumu cha mazungumzo ya kina na ya muda mrefu.