Feb 25, 2016 08:02 UTC
  • Kerry aisihi Seneti ya US kutopitisha vikwazo vipya dhidi ya Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amelishauri Bunge la Seneti la nchi hiyo lisipitisha vikwazo vipya dhidi ya Iran na badala yake kutoa fursa kwa utekelezwaji wa makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Tehran na kundi la 5+1 mwaka uliopita.

John Kerry amewaambia wanachama wa kamati ya Seneti inayohusika na masuala ya nje kwamba vikwazo vipya dhidi ya Iran vitaifanya Marekani kuonekana kama taifa lisilotekeleza ahadi zake za kimataifa.

Hii ni katika hali ambayo, Seneta wa jimbo la South Carolina, Lindsey Graham, amesema ameandaa orodha ya vikwazo vipya dhidi ya Iran kutokana na eti kupanuka uwezo wa Tehran katika uga wa makombora ya balistiki.

Wanasiasa wengine wa Marekani kutoka chama cha Republican wanashinikiza kuwekwa vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa kisingizio cha eti rekodi mbaya ya haki za binadamu hapa Iran. Hii ni katika hali ambayo, Marekani inahesabiwa na mashirika mengi ya kimataifa kuwa mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu kutokana na kuendesha mateso dhidi ya wafungwa katika jela za Abu Ghuraib na Guantanamo na vilevile kuwabagua Wamarekani wenye asili ya Afrika.

Tags