Iran ni ya kwanza kwa maendeleo ya kielimu katika ulimwengu wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i25108-iran_ni_ya_kwanza_kwa_maendeleo_ya_kielimu_katika_ulimwengu_wa_kiislamu
Mashirika ya kimataifa ya viwango ya ISI na Scopus yamesema katika ripoti zao kwamba Iran inashikilia nafasi ya kwanza ya maendeleo ya sayansi na teknolojia katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu.
(last modified 2026-02-25T07:04:48+00:00 )
Feb 14, 2017 03:16 UTC
  • Iran ni ya kwanza kwa maendeleo ya kielimu katika ulimwengu wa Kiislamu

Mashirika ya kimataifa ya viwango ya ISI na Scopus yamesema katika ripoti zao kwamba Iran inashikilia nafasi ya kwanza ya maendeleo ya sayansi na teknolojia katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu.

Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amethibitisha habari hiyo na kufafanua kwa kusema: Nafasi ya maendeleo ya kielimu ya Iran ni ya 16 ulimwenguni kwa mujibu wa taasisi mbili za viwango za kimataifa za Scopus na ISI na ni ya kwanza katika eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu.

Mohammad Farhadi, alisema hayo jana (Jumatatu) wakati wa sherehe za kufunga tamasha la 30 la kimataifa la Kharazmi hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, vyuo vikuu 14 vya Iran vimo katika orodha ya vyuo vikuu bora kwa mujibu wa viwango vya "Leiden" huku wasomi 200 wa Iran wakiwa katika daraja ya kwanza kati ya wasomi na wanasayansi wakubwa duniani.

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia nchini Iran

 

Waziri wa Sayansi wa Iran amesema, katika hali ambayo, ukuaji wa kielimu duniani mwaka 2015 ulikuwa umepanda kwa asilimia sita ikilinganishwa na mwaka 2014, nchini Iran wastani wa kiwango cha ukuaji wa maendeleo ya kielimu ulikuwa ni sawa na asilimia 17 na nusu.

Amesema, karibu mashirika elfu moja ya elimu za kimsingi katika vijiji 39 vya elimu na teknolojia viko nchini Iran ambapo katika miaka miwili ya 2014 na 2015 yamezalisha zaidi ya dola milioni 100 za Kimarekani kwa kuuza elimu.

Aidha amesema, hivi sasa kuna miradi 235 inayoendeshwa kwa ushirikiano wa vyuo vikuu mbalimbali muhimu na kiwango cha makala za kielimu kilichotolewa mwaka jana kiliongezeka kwa asili tano ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.