Qassemi: Zama za kutumia vitisho vya kijeshi zimepita
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa vitisho vya kutumia nguvu za jeshi vilivyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Venezuela na kusisitiza kuwa uzoefu unaonesha kuwa, zama za kutumia vitisho vya kijeshi na mashinikizo dhidi ya nchi huru na zinazojitawala kwa ajili ya kuzilazimisha zikubali matakwa yasiyo ya kimantiki na haramu zimemalizika.
Bahram Qassemi malaani matamshi ya kichochezi yaliyotolewa na Rais wa Marekani kuhusu matukio ya Venezuela na kusema ni kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amepinga uingiliaji kati wa kigeni katika masuala ya Venezuela na kusisitiza udharura wa kuheshimiwa utawala na mamlaka ya nchi hiyo chini ya sheria cha kimataifa.
Ijumaa iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alidai kwamba, kuna machaguo mengi kuhusu Venezuela mezani kwake ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya nchi hiyo.