Usalama Iran unatokana na umoja wa Mashia na Masuni
(last modified Sat, 02 Sep 2017 02:28:29 GMT )
Sep 02, 2017 02:28 UTC
  • Usalama Iran unatokana na umoja wa Mashia na Masuni

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu Iran amesema usalama uliopo hivi sasa nchini umetokana na umoja na mshikamano uliopo baina ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni.

Hussein Ali Amiri, Makamu wa Rais wa Iran katika masuala ya Bunge aliyasema hayo Ijumaa wakati akizungumza katika Sala ya Idul Adha  ya Waislamu wa Kisuni katika mji wa Gonbad-e Kāvus katika mkoa wa Golestan, kaskazini mwa Iran. Amesmea pamoja na kuwepo ukosefu wa usalama katika eneo la Asia Magharibi na kuwepo makundi ya magaidi wakufurishaji kama vile ISIS au Daesh, umoja na mshikamano wa Mashia na Masuni pamoja na kujitolea vikosi vya usalama ni nukta ambazo zimechangia kuwepo usalama mkubwa nchini Iran.

Aidha amesema Wairani wa kaumu za Turkman katika mkoa wa Golestan wamethibitisha mara kadhaa kuwa, kila wakati Uislamu na Mapinduzi ya Kiislamu Iran yanapokuwa hatarini, wao hujitokeza katika medani na kutetea malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Sala ya Idul Adha Golestan kaskazini mwa Iran, September 1, 2017

Sala ya Idul Adha ilisaliwa kote Iran jana Ijumaa na kuhudhuriwa kwa wingi na waumini ambapo pia wengi wametekeleza amali muhimu ya siku hiyo ya kuchinja.

Jana Ijumaa 10 Dhul Hijja mwaka 1438 sawa na Septemba Mosi ilikuwa Sikukuu ya Idul Adha kote duniani.