Rais Rouhani na Erdogan wamepinga kura ya maoni ya kujitenga Kurdistan, Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i34819-rais_rouhani_na_erdogan_wamepinga_kura_ya_maoni_ya_kujitenga_kurdistan_iraq
Marais Hassan Rouhani wa Iran na Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki wamefanya mazungumzo ya simu wakipinga katakata kura ya maoni inayofanyika katika eneo la Kurdistan kwa ajili ya kujitenga eneo hilo na Iraq na kutilia mkazo udharura wa kulindwa umoja wa ardhi yote ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 25, 2017 03:41 UTC
  • Rais Rouhani na Erdogan wamepinga kura ya maoni ya kujitenga Kurdistan, Iraq

Marais Hassan Rouhani wa Iran na Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki wamefanya mazungumzo ya simu wakipinga katakata kura ya maoni inayofanyika katika eneo la Kurdistan kwa ajili ya kujitenga eneo hilo na Iraq na kutilia mkazo udharura wa kulindwa umoja wa ardhi yote ya nchi hiyo.

Katika mazungumzo hayo, Rais Rouhani ameeleza kuridhishwa na ushirikiano wa pande hizo mbili na kusema: Ni suala muhimu sana kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kulindwa ardhi na umoja wa kitaifa wa Iraq na vilevile usalama wa eneo la Mashariki ya Kati na kuna ulazima wa kutoa ujumbe wa wazi kwa upande wowote unaotaka kuvuruga amani na usalama wa eneo hilo. 

Amesema misimamo ya Iran na Uturuki kuhusu kura ya maoni ya Kurdistan inaoana kikamilifu na kuongeza kuwa, nchi za eneo hili hazitaruhusu jaribio la aina yoyote la kuanzisha machafuko mapya.

Ramani ya Iraq

Kwa upande wake Rais Recep Tayyep Erdogan amesema kuwa, serikali yake imejadili suala la kuchukua hatua za lazima za kisiasa, kiuchumi na hata kijeshi za kukabiliana na suala hilo.

Kiongozi wa mamlaka ya utawala wa ndani katika eneo la Kurdistan huko kaskazini mwa Iraq, Masudi Barazani ameshikilia msimamo wake wa kuitisha kura ya maoni ya kujitenga na Iraq iliyopangwa kufanyika hii leo licha ya upinzani mkubwa wa jamii ya kimataifa na nchi zote jinari na Iraq.