Ayatullah Araki: Umoja ni ufumbuzi wa matatizo ya jamii ya Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i37951-ayatullah_araki_umoja_ni_ufumbuzi_wa_matatizo_ya_jamii_ya_kiislamu
Katibu Mkuu wa Jumuuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, njia na utatuzi wa matatizo ya jamii ya Kiislamu na kupoza maumivu ya majeraha yaliyopo ni kuweko umoja na mshikamano baina ya Waislamu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 23, 2017 02:42 UTC
  • Ayatullah Araki: Umoja ni ufumbuzi wa matatizo ya jamii ya Kiislamu

Katibu Mkuu wa Jumuuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, njia na utatuzi wa matatizo ya jamii ya Kiislamu na kupoza maumivu ya majeraha yaliyopo ni kuweko umoja na mshikamano baina ya Waislamu.

Ayatullah Mohsen Araki amesema hayo katika mji wa Qum kusini mwa Tehran ambapo sambamba na kubainisha umuhimu wa umoja katika jamii ya Kiislamu ameongeza kuwa, umoja katika jamii ya Kiislamu ni ishara ya rehma ya Mwenyezi kama ambavyo hitilafu, mizozo na chuki ni ishara ya adhabu ya Mwenyezi ya Mungu.

Katibu Mkuu wa Jumuuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu ameashiria kufanyika Mkutano wa Kimataifa wa 31 wa Umoja wa Kiislamuu hapa mjini Tehran na kusisitiza kwamba, karibu wawakilishi kutoka nchi 70 duniani walishiriki katika mkutano wa mwaka huu na kuundwa Baraza la Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi za Kiislamu yalikuwa moja ya mafanikio muhimu ya mkutano huo.

Mkutano wa 31 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu

Kwa mujibu wa Ayatullah Araki, imeafikiwa kwamba, mawaziri sita wa zamani wa mashauri ya kigeni na wa sasa wa nchi za Kiislamu wanaounda kamati hiyo watakuwa wakifuatilia masuala muhimu yanayojiri katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Mkutano wa 31 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu  ulifanyika hapa mjini Tehran kuanzia 5 hadi 7 ya mwezi huu wa Desemba.