Sep 21, 2024 12:42 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Kujenga umma; somo muhimu zaidi la Mtume (SAW)

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya nafasi ya watu maalumu katika uundaji wa Umma wa Kiislamu na umoja wa ulimwengu wa Kiislamu na kubainisha kwamba, kwa kuundwa Umma wa Kiislamu, Waislamu kwa nguvu zao za ndani wanaweza kuondoa donda la saratani na khabithi la utawala wa Kizayuni kutoka Palestina na kusambaratisha ushawishi na uingiliaji wa mabavu wa Marekani katika eneo.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo kwa mnasaba wa kumbukizi ya kuzaliwa Mtume Muhammad SAW na Imamu Ja'far Swadiq AS katika hadhara ya maafisa wa serikali, mabalozi wa nchi za Kiislamu na wageni wa mkutano wa 38 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu na kueleza kwamba,  mbinu za Mtume za ulinganiaji zilitofautiana katika vipindi mbalimbali na kuongeza kuwa, Mtume ametoa somo kamili, jumuishi na la pande zote kwa maisha, ambapo moja ya mafunzo makubwa ya kinabii kwetu  ni ujenzi na uundaji wa Umma wa Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyazingatia mapambano ya miaka 13 ya Mtume (SAW) huko Makka na taabu, matatizo, njaa na kujitolea pakubwa katika zama hizo na baada ya hapo katika kipindi cha Hijra kuwa ni jiwe la msingi la kuunda Umma wa Kiislamu na akasema: Leo kuna nchi nyingi za Kiislamu na Waislamu wapatao bilioni mbili wanaishi duniani, lakini kundi hili haliwezi kuitwa "Umma" kwa sababu Umma ni kundi linaloelekea kwenye lengo moja, kwa uratibu na kwa hamasa, lakini Waislamu wa leo wamegawanyika.

Baadhi ya hadhirina wakimsimkiliza Kiongozi Muadhamu

 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza tena ulazima wa kukatwa kikamilifu uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi za Kiislamu na utawala wa Kizayuni na kuongeza kuwa: Nchi za Kiislamu pia zinapaswa kudhoofisha kikamilifu uhusiano wa kisiasa na utawala wa Kizayuni na wakati huo huo kuimarisha mashambulizi ya kisiasa na vyombo vya habari na kuonyesha wazi na bayana kabisa kwamba, wako pamoja na taifa la Palestina.

Tags