Iran na Senegal kuimarisha ushirikiano wao katika uga wa sayansi
Jamhuri ya Kiislamu na Iran na Senegal zimeazimia kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika nyuga mbalimbali na hususan ushirikiano wao katika uga wa sayansi.
Hossein Salar Amoli, Kaimu Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Sayansi wa Iran ametoa mwito wa kuanzishwa tawi la Shirika la Mafunzo ya Kiufundi ya Iran katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, waziri huyo wa Iran ametoa mwito huo katika walipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Senegal nchini, Baba Karba hapa mjini Tehran.
Kadhalika amemtaka balozi huyo wa Senegal kuandaa mazingira ya kwenda nchini humo wasomi na wanaakademia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili nchi hiyo ya Kifrika ipate kustafidi na uzoefu na tajriba ya wasomi hao wa sayansi wa hapa nchini.
Kwa upande wake, Balozi wa Senegal hapa nchini, Baba Karba ameeleza juu ya kuridishwa nchi yake na ushirikiano wa hivi sasa wa nchi yake na Iran katika masuala ya kisayansi, huku akipongeza uhusiano wa kipekee wa nchi mbili hizi katika uga wa utamaduni.
Aprili mwaka huu, Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran aliitembelea Dakar, ambapo katika mazungumzo yake na maafisa wa Senegal alijadili suala la kurahisisha njia za mawasiliano na ushirikiano wa wafanyabiashara wa Iran na Senegal.
Aidha waijadili kuhusu ushirikiano wa kiuchumi hususan katika masuala ya huduma za kiufundi na kihandisi, utengenezaji wa magari, mafuta na petrokemikali, umeme, bidhaa za chakula na teknolojia ya kisasa.