Mazungumzo ya Dakta Zarif na Rais Sauli Niinistö wa Finland mjini Helsinki
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55473-mazungumzo_ya_dakta_zarif_na_rais_sauli_niinistö_wa_finland_mjini_helsinki
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo mjini Helsinki na Rais Sauli Niinisto wa Finland na kujadili masuala ya kieneo na kimataifa.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Aug 19, 2019 07:12 UTC
  • Mazungumzo ya Dakta Zarif na Rais Sauli Niinistö wa Finland mjini Helsinki

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo mjini Helsinki na Rais Sauli Niinisto wa Finland na kujadili masuala ya kieneo na kimataifa.

Dakta Muhammad Javad Zarif jana usiku aliwasili Helsinki mji mkuu wa Finland akiuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo amekutana na kufanya mazungumzo pia na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo.

Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran alitarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ustawi na Ushirikiano wa Kibiashara wa nchi hiyo ya bara Ulaya.

Kujadili masuala ya pande mbili, ushirikiano wa Iran na Ulaya, masuala ya kieneo na kimataifa, kulindwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na utekelezwaji wa mfumo maalumu wa mabadilishano ya fedha kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya, kwa kifupi INSTEX ni miongoni mwa ajenda kuu za mazungumzo ya Dakta Zarif na viongozi wa Finland.

Mazungumzo ya ujumbe wa kisiasa wa Iran na viongozi wa Finland

Mara baada ya kukamilisha safari yake nchini Finland, Dakta Muhammad Javad Zarif anatarajiwa kuzitembelea pia nchi za Norway na Sweden.

Jana alipowasili Helsinki, mji mkuu wa Finland, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwaambia waandishi wa habari kwamba, Iran ni muhimu kwa Ulaya na kusisitiza udharura wa madola ya Ulaya kutekeleza ahadi zake kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.