Uimarishaji wa wastani wa uhusiano; mhimili wa udiplomasia wa Iran
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa na lengo la kukabiliana na vita vya kiuchumi vya Marekani ina machaguo kadhaa.
Moja ya machaguo hayo ni kutumia uwezo wa ndani kwa ajili ya kustawisha uchumi na wakati huo huo kuwa na anuai ya mahusiano ya kiuchumi yenye mlingano sambamba na kustafidi na fursa na uwezo wa ushirikiano wa kieneo. Katika uwanja huo, utendaji mbalimbali katika mahusiano ya nje ya Iran umezingatiwa ambapo duru za habari na za kisiasa zinalitaja hilo kama diplomasia ya kiuchumi ya Iran mkabala na vikwazo vya Marekani.
Kwa mtazamo wa weledi wa masuala ya kisiasa na kiuchumi ni kuwa, ili uwezo wa ndani uwe amilifu kwa ajili ya ustawi wa uchumi, kuna ulazima wa kustafidi na fursa na uwezo wa kieneo. Katika fremu hiyo, diplomasia ya kiuchumi ya Iran mbali na kupanua uhusiano wa pande mbili, imejikita pia katika kuimarisha mitazamo ya pamoja ya kieneo na ushirikiano na jumuiya za kieneo kama Jumuiya ya Kiuchumi ya Eurasia, Jumuiya ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN), Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ECO na Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi.
Safari ya ujumbe wa kisiasa na kiuchumi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika wiki za hivi karibuni ikiwemo safari ya Dakta Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran barani Asia ambaye kwa sasa yupo nchini Bangladesh, zinatathminiwa katika fremu hii. Katika safari hiyo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, mbali na kuwa na mazungumzo na viongozi wa Bangladesh anatarajiwa pia kushiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi na kuhutubia katika mkutano huo.
Baada ya kukamiilisha safari yake nchini Bangladesh, Dakta Zarif anatarajiwa kuelekea nchini Indonesia ambapo akiwa huko atafanya mazungumzo na viongozi wa nchii hizo kuhusiana na uhusiano wa pande mbili pamoja na matukio ya Ulimwengu wa Kiislamu.
Safari ya Dakta Zarif nchini Bangladesh na kushiriki kwake katika mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi sambamba na mwenendelezo wa safari yake huko Indonesaia, ina nukta mbili muhimu.
Umuhimu wa kwanza ni mazungumzo katika fremu ya uhusiano wa pande mbili wa Iran na nchi mbili za Kiislamu katika uga wa uhusiano wa kibara. Kwa muktadha huo, safari hiyo ni fursa ya kufuatilia malengo ya pamoja ya kiuchumi na kibiashara. Umuhimu wa pili ni kushiriki Dakta Zarif hapo kesho Alkhamisi katika mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi, utakaofanyika Dakar mji mkuu wa Bangladesh.
Viongozi wa ngazi za juu wa eneo hilo kubwa kijiografia wanatarajiwa kuhudhuria katika mkutano huo wa tano wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi. Jumuiya hiyo ina nchi wanachama 19 kutoka mabara matatu ya Asia, Afrika na Oceania ikiwa na wakazi zaidi ya bilioni mbili.
Ali Sabagheyan, mhadhiri wa Chuo Kikuu na mtafiti wa mahusiano ya kimataifa anazungumzia umuhimu na nafasi ya Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Bahari ya Hindi kwa kusema:
Jumuiya hii ambayo kimsingi inafahamika kama ubunifu wa Ukanda wa Bahari ya Hindi imejikita zaidi katika kuimarisha ustawi wa kudumu na wenye mlingano katika eneo baina ya nchi wanachama. Ni kwa kuzingatia hilo, ndio maana jumuiya hii imekuwa na nafasi muhimu katika kupanua biashara huru na kuondoa vizingiti vilivyoko katika harakati ya biashara, uwekezaji vitega uchumi na teknolojia katika eneo la Bara Hindi.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ipo katika mazingira nyeti na wakati huo huo huo tata na yenye kuanisha hatima na mustakbali wa mambo. Vikwazo na mashinikizo ya kidhulma ya kimataifa dhidi ya Iran kwa hakika yanatokana na kusimama kidete taifa hili katika kutetea haki zake na kutokubali kunyongeshwa. Hali hii imeufanya mwenendo wa ustawi wa kiuchumi wa nchi hii kukabiliwa na vizingiti. Kutumia wenzo wa vikwazo, kushadidisha mashinikizo ya kimataifa na kufanyika njama za kuitenga Iran ni mikakati mitatu mikuu ya Marekani katika hali ya hivi sasa.
Hata hivyo kuvivukka vizingiti hivyo sio jambo gumu kama ilivyokuuwa huko nyuma kwani bila shaka kuna machaguo mengi mbele ya Iran ambapo kwa kuyatumia taifa hili linaweza kuvishinda vizuizi hivyo. Moja ya mambo muhimu ya kuvuka vizingiti hivyo katika mazingira ya sasa na kukabiliana na ugaidi wa kiuchumi wa Marekani ni uimarishaji wa wastani wa uhusiano wa nje na wa kiuchumi jambo ambalo kwa sasa limo katika ajenda za siasa za kigeni za Iran. Ukweli ni kuwa, hatua ya Iran ya kutekeleza kwa umakini siasa za kigeni sambamba na kutetea haki zake katika uga wa kimataifa inalenga kusimama kidete mkabala na mfumo wa kibeberu duniani.