Zarif asisitiza juu ya kushindwa siasa za Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa mgogoro wa Yemen utamalizika iwapo njia za ufumbuzi zilizopendekezwa na Iran zitakubaliwa.
Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemhutubu Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani akisema kuwa: Washington sasa imejielekeza katika siasa za upotoshaji wa hali ya juu baada ya kushindwa siasa zake za mashinikizo ya kiwango cha juu. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Marekani na satalaiti zake zimekwama huko Yemen huku ikiwa na njozi kwamba, kuwa na nguvu ya silaha kutaipatia ushindi wa kijeshi.
Zarif amesema kuwa, hatua ya kuituhumu Iran kuwa ndiyo mkosa haitapelekea kumalizika maafa ya Yemen bali kinyume chake, mgogoro wa nchi hiyo unaweza kukomeshwa iwapo mapendekezo ya Iran yatakubaliwa ili kuhitimisha vita na kuandaa mazingira ya kufanyika mazungumzo nchini humo.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani alidai hivi karibuni katika radiamali yake kwa shambulio lililofanywa na wapiganaji wa kujitolea wa Yemen katika vituo vya mafuta vya Saudi Arabia kwamba: Tehran inaunga mkono mashambulizi ya Wayemeni dhidi ya maeneo ya Saudia.