Spika wa Bunge la Iran asisitiza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia (JCPOA)
(last modified Thu, 28 Apr 2016 15:16:59 GMT )
Apr 28, 2016 15:16 UTC
  • Spika wa Bunge la Iran asisitiza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia (JCPOA)

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesisitiza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1 yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).

Dakta Ali Larijani, ametoa sisitizo hilo leo alipohutubia semina ya taifa ya mabadiliko ya jiopolitiki katika eneo la Magharibi mwa Asia lililofanyika hapa mjini Tehran.

Spika wa Bunge ameashiria hotuba ya jana ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu makubaliano na nyuklia na kueleza kwamba Wamagharibi hawaaminiki, lakini kama hawatatekeleza ahadi zao, Jamhuri ya Kiislamu itatumia nyenzo zake zitakazowafanya walazimike kutekeleza ahadi hizo.

Kuhusiano na hali ya eneo la Mashariki ya Kati na hatari ya ugaidi, Larijani amesena Wamagharibi hawana nia ya dhati ya kupambana na ugaidi.

Spika wa Bunge amebainisha kuwa moja ya matatizo makubwa katika eneo ambalo limezushwa na vibaraka wa Marekani na lisilo na uhalisia ni vita vya kimadhehebu na kuongezea kwa kusema nchi za eneo nazo zimeisaidia Marekani katika suala hilo ili kufikia malengo yake.

Dakta Larijani amebainisha kuwa kinachofuatiliwa na Wamarekani na Magharibi ni kupora mafuta na maliasili za nchi za eneo.../

Tags