Apr 13, 2021 07:25 UTC
  • Iran yawapongeza Waislamu kwa kuwadia mwezi wa Ramadhani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewapongeza na kuwatakia Waislamu wote duniani kheri na baraka kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Mohammad Javad Zarif ameandika: Pongezi kwa Waislamu wote duniani, kwa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa wema, amani, baraka, na sadaka.

Ameongeza kuwa: Tunamuomba Allah Mtukufu Atupe umoja na mshikamano Waislamu mkabala wa changamoto, ili mataifa tofauti ya Kiislamu yafikie maslahi ya pamoja katika mwezi huu, na yapaze sauti ya ukweli na haki miongoni mwa watu, na yaondokane na dhulma za madhalimu.

Mwezi mwandamo wa kuashiria kuanza mwezi mpya

Nchi za Indonesia, Uturuki, Mauritania, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), Bahrain, Kuwait, Palestina, Misri, Oman, Jordan, Lebanon na Tunisia ni miongoni mwa nchi za Kiislamu zilizoanza funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani hii leo.

Wakati huo huo, baadhi ya mataifa ya Kiislamu yametangaza kuwa, Jumatano ya kesho itakuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Tags