Iran: Hatuko tayari kufanya mazungumzo chini ya vitisho na mashinikizo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91342-iran_hatuko_tayari_kufanya_mazungumzo_chini_ya_vitisho_na_mashinikizo
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: viongozi wa Marekani wanajua kwamba Iran haiko tayari kufanya mazungumzo na kuridhia kutoa fursa kwa mashinikizo na vitisho, kwa sababu mapatano yana mantiki yake; na msimamo wa Iran kuhusiana na mazungumzo ya JCPOA uko wazi kabisa.
(last modified 2026-05-06T11:35:21+00:00 )
Dec 05, 2022 07:34 UTC
  • Iran: Hatuko tayari kufanya mazungumzo chini ya vitisho na mashinikizo

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: viongozi wa Marekani wanajua kwamba Iran haiko tayari kufanya mazungumzo na kuridhia kutoa fursa kwa mashinikizo na vitisho, kwa sababu mapatano yana mantiki yake; na msimamo wa Iran kuhusiana na mazungumzo ya JCPOA uko wazi kabisa.

Nasser Kanaani, ameeleza hayo leo katika mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari alipoashiria misimamo tofauti ya Wamarekani kuhusiana na Iran na akasema: kipaumbele cha Marekani si mazungumzo, bali imejikita kwenye masuala mengine.
Kanaani ameongeza kuwa: kuna mgongano wa kauli na matendo katika misimamo ya wanachama wa Magharibi wa JCPOA na hasa hasa serikali ya Marekani; zaidi ukiwa ni undumakuwili katika matendo na kutoheshimu wala kutekeleza Marekani majukumu yake katika JCPOA, hali ambayo imevuruga mwenendo wa makubaliano ya JCPOA. Amesema, hali hiyo imepelekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ishindwe kufaidika na fursa na manufaa ya kiuchumi ya JCPOA, na vilevile kuvuruga hatua za pande kadhaa kimataifa za kuyapatia ufumbuzi masuala tata na yenye kutiliwa shaka kimataifa.
Image Caption

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ameeleza pia kwamba, hayo ni matokeo ya utendaji mbaya wa serikali ya Marekani, ambayo inapaswa kubeba dhima na kuwajibika kwa mwenendo na vitendo vyake visivyo vya uwajibikaji kuhusiana na suala hilo.

Kanaani amesisitiza pia kuwa: Iran iliheshimu na kutekeleza majumu yake katika JCPOA; na serikali ya Marekani ndiyo iliyokanyaga na kukiuka makubaliano hayo; na kuhusiana na hilo, nchi za Ulaya ambazo ni wanachama wa JCPOA nazo pia hazikutekeleza wajibu wao, wala hazikuweza kufidia hasara zilizotokana na hatua ya upande mmoja ya Marekani ya kujitoa kinyume cha sheria katika JCPOA.
Pamoja na hayo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ameongezea kwa kusema: Iran ingali na msimamo thabiti wa utayarifu kuhusiana na mchakato wa mazungumzo.../