Rais Raisi: Mahesabu ya adui katika njama ya karibuni yameenda kombo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91770-rais_raisi_mahesabu_ya_adui_katika_njama_ya_karibuni_yameenda_kombo
Rais Ebrahim Raisi amesema: kutokana na basira na kuwa macho wananchi wa Iran, mahesabu ya adui katika njama ya karibuni yameenda kombo sawa na ilivyokuwa katika fitna za huko nyuma.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 16, 2022 08:30 UTC
  • Rais Raisi: Mahesabu ya adui katika njama ya karibuni yameenda kombo

Rais Ebrahim Raisi amesema: kutokana na basira na kuwa macho wananchi wa Iran, mahesabu ya adui katika njama ya karibuni yameenda kombo sawa na ilivyokuwa katika fitna za huko nyuma.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo alipohutubia mkutano wa hadhara wa matabaka mbalimbali ya wananchi wa Nahbandan katika Mkoa wa Khorasan Kusini (mashariki ya Iran) na akaeleza kuwa basira na kuwa macho wananchi wa Iran ya Kiislamu kumevuruga mipango ya maadui. Amefafanua kwa kusema: sababu inayopelekea adui asiweze kuivamia nchi licha ya njama na fitna zote anazofanya ni kujitokeza wananchi katika medani mbalimbali za kisiasa na kijamii.
Rais Ebrahim Raisi akihutubia wananchi wa Nahbandan

Sayyid Ebrahim Raisi amesema, kwa mujibu wa takwimu rasmi za vyombo vya habari vya Magharibi, mamia ya wanawake wanauliwa na polisi wa Marekani kila mwaka na akaongeza kuwa: Marekani na washirika wake hawawezi kuunga mkono haki za binadamu, ambazo mfano wa wazi wa ukiukwaji wake ni kukanyagwa haki za wananchi wasio na hatia wa Palestina na Yemen.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema pia kuwa, kundi la kigaidi la DAESH (ISIS) liliundwa na Wamagharibi na akafafanua kwamba: sababu ya wananchi wa Iran ya Kiislamu kusema "Mauti kwa Marekani" ni jinai za kigaidi inazofanya na kuua watu wasio na hatia ikiwemo jinai ya kigaidi ya Shahcheragh mjini Shiraz, kusini mwa Iran.
Rais Raisi amesisitiza pia kwamba maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayatasimama, na akaongezea kwa kusema: "miji na nchi imejengwa na wanaume na wanawake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran; na baada ya sasa pia ndivyo itakavyoendelea kujengwa; sisi hatujaweka matumaini wala matarajio yoyote kwa maajinabi".../