Rais Raisi: Zaidi ya 90% ya dawa zinazohitajika zinatengenezwa nchini
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i93220-rais_raisi_zaidi_ya_90_ya_dawa_zinazohitajika_zinatengenezwa_nchini
Rais Ebrahim Raisi amesema, asilimia tisini ya dawa zinazohitajika zinatengenezwa humuhumu nchini.
(last modified 2026-05-06T11:35:21+00:00 )
Jan 23, 2023 08:39 UTC
  • Rais Raisi: Zaidi ya 90% ya dawa zinazohitajika zinatengenezwa nchini

Rais Ebrahim Raisi amesema, asilimia tisini ya dawa zinazohitajika zinatengenezwa humuhumu nchini.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mafanikio iliyopata Iran katika nyanja za tiba hususan kutengeneza asilimia 90 ya dawa zinazohitajika ndani ya nchi na uwezo wa kutengeneza na kusafirisha chanjo nje ya nchi na akasema: "inapasa tudumishe na kuinua uwezo wa nchi kuwa marejeo ya kisayansi na kufikiria jinsi ya kuongeza kiwango cha ufanisi".
 
Seyyid Ebrahim Raisi ametoa sisitizo hilo leo katika Tamasha la 28 la Utafiti na Teknolojia ya Sayansi ya Tiba ya Razi, ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano ya Viongozi na akaongezea kwa kusema: "tunawapongeza watafiti na wahakiki walioleta mafanikio katika uzalishaji".
Rais Raisi akihutubia Tamasha la Utafiti na Teknolojia ya Sayansi ya Tiba ya Raz

Katika hafla hiyo, washindi wa Tamasha la 28 la Utafiti na Teknolojia ya Sayansi ya Tiba ya Razi walizawadiwa tuzo katika sehemu mbili za watafiti halisi na majimui rasmi za utafiti.

 
Akigusia mkutano wake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pembezoni mwa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Raisi amesema: "katika mazungumzo hayo (Guterres) aliomba radhi mara kadhaa kwamba alijaribu kuzuia vikwazo vya dawa dhidi ya Iran, lakini hakufanikiwa".
 
Aidha, Seyyid Ebrahim Raisi amesema: "nilimsisitizia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa, leo mbali na kwamba zaidi ya 70% ya watu wa Iran wamechanjwa chanjo ya kinga ya corona, wataalamu wa Iran wamefanikiwa pia kutengeneza chanjo sita na sasa hatuagizi tena chanjo kutoka nje".
 
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha pia kwa kusema: "wanasayansi wa Kiirani wamefanya jitihada usiku na mchana kuleta heshima hiyo ya kujivunia kwa nchi, ili tuwe moja ya watengenezaji chanjo ulimwenguni".../