-
Mwakilishi wa US adai vita vya Israel dhidi ya Lebanon haviepukiki ikiwa Hizbullah haitapokonywa silaha
Oct 20, 2025 06:10Tom Barrack, balozi wa Marekani nchini Uturuki na mjumbe maalumu wa masuala ya Syria, ametoa onyo la kutisha kwa Lebanon akiitaka ama iipokonye silaha Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya nchi hiyo Hizbulla au ikabiliwe na mashambulizi mengine ya Israel na migogoro ya kiuchumi na kisiasa.
-
Trump azitaka Russia na Ukraine zisimamishe vita mahali zilipo sasa hivi kwenye medani ya mapigano
Oct 20, 2025 06:10Rais wa Marekani Donald Trump ametoa wito kwa Russia na Ukraine kusimamisha vita katika mstari wa mapigano zilipo hivi sasa, pendekezo ambalo litaiwezesha Moscow kuhodhi sehemu kubwa ya maeneo ya ardhi ya Ukraine.
-
Ulimwengu wa Spoti, Okt 20
Oct 20, 2025 03:32Hujambo msikilizaji mpenzi, nina wingi wa matumaini kwamba u mzima wa afya. Karibu tuangazie japo kwa ufupi, baadhi ya matukio makubwa yaliyojiri viwanjani katika muda wa siku zilizopita, kitaifa, kieneo na kimataifa. Nakusihi usibanduke hapo ulipo hadi tamati ya kipindi….
-
Meja Jenerali Pakpour: Iran iko tayari kikamilifu kuimarisha uhusiano wa kistratejia na Yemen
Oct 20, 2025 03:14Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limesema kuwa limejiandaa kikamilifu kukuza ushirikiano wa kimkakati na vikosi vya ulinzi vya Yemen katika mapambano dhidi ya mabeberu wa dunia na Uzayuni wa kimataifa.
-
Iran yalaani kitendo cha Israel cha kumtesa mwanaharakati Greta Thunberg
Oct 20, 2025 03:13Esmail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kumtesa mwanaharakti wa haki za binadamu aliyedhihirisha mshikamano na watu wa Palestina. Baqaei amevitaja vitendo hivyo vya Israel kuwa vya ukatili, visivyo vya kibinadamu na vya udhalilishaji.
-
WHO: Mgonjwa wa mwisho wa Ebola Kongo aruhusiwa kutoka katika kituo cha matibabu
Oct 20, 2025 03:12Shirika la Afya Duniani (WHO) jana liliripoti kuwa mgonjwa wa mwisho wa Ebola aliruhusiwa jana kutoka kwenye kituo cha matibabu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
'Jukwaa la kufyatulia risasi' lanaswa katika eneo linalotazamana na ndege ya Trump
Oct 20, 2025 03:10Idara ya Huduma ya Siri ya Marekani imethibitisha kuwa imegundua jukwaa linalotiliwa shaka la kufyatulia risasi karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Palm Beach likiwa na uwezo wa kuona moja kwa moja mahali ambapo kwa kawaida Rais Donald Trump hutokea kwenye Air Force One.
-
Idara ya Vyombo vya Habari vya Serikali Gaza yasajili ukiukaji 80 wa Israel tangu kusitishwa mapigano
Oct 20, 2025 03:08Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali katika Ukanda wa Gaza imesema ukiukaji wa Israeli wa mapatano ya kusitisha vita unaakisi hamu ya utawaka huo vamizi ya kuzidisha machafuko na mtazamo wake wa kichokozi dhidi ya watu wa ukanda huo.
-
Trump anamtishia Rais wa Colombia, Petro ajibu mapigo: Soma kwa makini kuhusu nchi yetu
Oct 20, 2025 03:08Rais wa Marekani, Donald Trump amemshutumu Rais wa Colombia Gustavo Petro kwa kuhusika katika kuongezeka biashara ya dawa za kulevya, na kutishia kuingilia moja kwa moja Marekani nchini Colombia.
-
Ripoti: Asilimia 97 ya shule za Gaza zimeharibiwa kwa mashambulizi ya Israel
Oct 19, 2025 23:58Ripoti rasmi zinasema, mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel yameharibu asilimia 97 ya shule za Ukanda wa Gaza na hivyo kuhatarisha mustakbali wa kielimu wa wanafunzi laki tatu wa Kipalestina katika eneo hilo.