Apr 20, 2024 08:16 UTC
  • Harakati ya Kiislamu Iraqi yashambulia mji wa Eilat

Harakati ya Kiislamu ya Iraq imetangaza kuwa imeshambulia maeneo muhimu katika mji wa Eilat, ulioko kusini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Muqawama wa Iraq umesema kuwa umefanya operesheni dhidi ya kambi ya anga ya Ovda kusini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israeli.

Katika muendelezo wa kupinga mashambulizi ya utawala haramu wa Israel, kuunga mkono watu wetu huko Gaza na kukabiliana na mauaji yanayofanywa dhidi ya raia wa Palestina, wakiwemo watoto, wanawake na wazee, wapiganaji wa Muqawama wa Kiislamu nchini Iraq, tangu Jumatatu tarehe 15 Aprili 2024, walilenga Kambi ya Anga ya 'Ovda' ya Wazayuni katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drone), imesema taarifa ta Muqawama wa Iraq.

Ilimesema shambulio hilo ni kujibu mauaji yaliyofanywa na utawala haramu wa  Israel dhidi ya raia wa Palestina wakiwemo wanawake, watoto na wazee.

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu nchini Iraq imesema kuwa itaendeleza Ooperesheni zake dhidi ya maeneo ya utawala haramu wa  Israel.

Muungano wa makundi ya Muqawama nchini Iraq umekuwa ukifanya mashambulizi mengi kama hayo dhidi ya maeneo ya utawala wa Israel, tangu utawala huo unaoikalia kwa mabavu Palestina, uanzishe vita na mauaji ya halaiki huko ukanda wa  Gaza mwezi Oktoba 7.

 

Kikundi cha Harakati cha Kiislamu cha Iraq

 

Tangu kuanza kwa mashambulizi hayo, utawala huo haramu wa Israel umeua zaidi ya Wapalestina 34,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.