-
Gazeti la Saudia: Mahujaji wa Qatar wachague Hijja au kuuangusha utawala wa nchi yao
Aug 15, 2018 07:30Gazeti la Okaz la nchini Saudi Arabia limewataka mahujaji wa Qatar kuchagua moja kati ya mawili, ima kufanya ibada ya Hijja na kuunga mkono utawala wa Al Thani na kwamba iwapo wanataka kutekeleza ibada hiyo, basi wanatakiwa kwanza kuuondoa madarakani utawala huo.
-
Wairani zaidi ya elfu 80 wameelekea Makka kwa ajili ya ibada ya Hija
Aug 14, 2018 09:20Afisa wa msafara wa ibada ya Hija wa Iran amesema kuwa hadi kufikia Jumatatu ya jana karibu Wairani elfu 80 walikuwa wameelekea katika miji mitakatifu ya Makka na Madina kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija.
-
Mkuu wa Mahujaji wa Iran awataka Waislamu kutumia fursa ya Hija kuweka pembeni tofauti zao
Aug 13, 2018 14:53Mkuu wa mahujaji wa Iran amesema kuwa, ibada ya Hija ni fursa nzuri sana kwa Waislamu katika nyuga tofauti na amezitaka nchi za eneo hili kutumia vizuri fursa ya Hija kuweka pembeni hitilafu zao ndogodongo na kuungana katika kuurejeshea heshima na utukufu wake umma mzima wa Kiislamu.
-
Waislamu wa Canada waandamana kupinga hatua ya Saudia ya kuwazuia kwenda kuhiji Makka
Aug 12, 2018 14:48Waislamu nchini Canada wamefanya maandamano wakipinga siasa za utawala wa kifalme wa Saudi Arabia za kuwazuia kwenda kutekeleza ibada ya Hija katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.
-
Saudia yashitakiwa UN kwa kuingiza siasa katika ibada ya Hija
Jul 18, 2018 02:31Kamati ya Kimataifa ya Kusimamia Haram Mbili za Makka na Madina imewasilisha barua mbili tofauti kwa Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa na Kamisheni ya Kidini na Uhuru wa Kujieleza ya Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Bunge la Ulaya, ikiishitaki Saudi Arabia kwa kuingiza masuala ya siasa katika ibada ya Hija sambamba na kuweka mipaka ya uhuru wa kidini.
-
Ibada ya Kimaanawi na kisiasa ya Hija kwa mtazamo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Jul 17, 2018 07:49Wasimamiaji na wafanyakazi wa Idara ya Masuala ya Ibada ya Hija jana asubuhi walikutana na Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kukaribia ibada hiyo na kuanza mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu kuelekea katika ardhi ya wahyi.
-
Qatar kuiburuza Saudia mahakamani kwa tuhuma za kuingiza siasa katika ibada ya Hijah
Jul 04, 2018 04:24Serikali ya Qatar na katika mfululizo wa kufuatilia masuala ya kisheria na kimataifa dhidi ya nchi za Saudi Arabia, Imarati, Bahrain na Misri, imetangaza kwamba imefungua mashitaka dhidi ya Riyadh kutokana na serikali ya nchi hiyo kuingiza siasa katika ibada ya Hijjah.
-
Wairani 85,200 kwenda kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu
Jun 28, 2018 03:48Wairani 85,200 wanatazamiwa kwenda nchini Saudi Arabia kutekeleza ibada tukufu ya Hija mwaka huu.
-
Syria: Riyadh ingali inawazuia raia wetu kwenda kufanya Hija
Jun 23, 2018 07:25Serikali ya Syria imeukosoa vikali utawala wa Aal-Saud kwa kuingiza siasa katika amali tukufu ya Hija, ambapo Riyadh imewazuia raia wa Syria kwenda kutekeleza ibada hiyo kwa mwaka wa saba mfululizo.
-
Jumuiya ya Maimamu Tunisia: Saudia inatumia mapato ya Hija kushambulia nchi za Waislamu
Jun 22, 2018 03:46Jumuiya ya Maimamu wa Swala za Jamaa nchini Tunisia imetoa taarifa ikisisitiza kuwa Saudi Arabia inatumia mapato yanayotokana na ibada ya Hija kwa ajili ya kuzishambulia nchi nyingine za Kiislamu na imemtaka Mufti Mkuu wa nchi hiyo kusimamisha safari za kwenda kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu huko Saudia.