Pars Today
Mwakilishi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameifundisha dunia nzima muqawama na kusimama kidete.
Waislamu ya madhehebu ya Shia Tanzania, visiwani Zanzibar, Nigeria na Niger wamefanya marasimu, matembezi na vikao vya kuadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (AS).
Baada ya shirika la utangazaji la utawala wa kifalme wa Uingereza BBC kusambaza mkanda wa video uliojaa chuki na upotoshaji dhidi ya Waislamu hasa wa Kishia na dhidi ya matembezi ya Arubaini ya Imam Husain AS, banda hilo la propaganda la ufalme wa Uingereza limekumbwa na ukosoaji mkali. Ammar Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam Tanzania
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njama za Marekani za mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi ya taifa la Iran zimefeli na kwamba takwimu zote na moyo na utanashati wa taifa la Iran vinaonesha kuwa, kipindi cha mashinikizo ya kiwango cha juu kimeyoyoma.
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema Arubaini ya Imam Hussein AS inabeba ujumbe muhimu wa mahaba, umoja na mshikamano wa Waislamu kote duniani mbele ya madola ya kibeberu.
Wanajeshi wa Nigeria wameushambulia msafara wa Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa wakishiriki katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein AS, viungani mwa mji mkuu wa nchi Abuja, na kuua shahidi kumi miongoni mwa waumini hao.
Maandamano ya mamilioni ya watu katika Arubaini ya Imam Husain AS na wajibu wa kuimarishwa kadiri inavyowezekana uhusiano wa Tehran na Baghdad ndiyo ajenda kuu ya mazungumzo ya simu yaliyofanywa baina ya mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Iraq.
Jana Ijumaa mwezi 20 Mfunguo Tano Safar sawa na tarehe 10 Novemba 2017 ilisadifiana na Arubaini ya Imam Husain AS kwa mujibu wa kalenda ya Iraq. Mamilioni ya Waislamu kutoka kona mbalimbali za dunia wameshiriki katika kumbukumbu hizo zilizofikia kileleni jana huko Karbala Iraq. Mwenzetu Salumu Bendedra aliyetumwa maalumu kuakisi tukio hilo ametutayarishia ripoti ifuatayo
Kumbukumbu za Arubaini ya Imam Husain ambazo hufikia kileleni mwezi 20 Mfunguo Tano Safar kila mwaka huko Karbala Iraq, zinawajumuisha pamoja mamilioni ya wapenzi wa Ahlul Bayt AS kutoka kona zote za dunia.
Polisi nchini Nigeria imetumia mabomu ya gesi ya kutoa machozi kuvunja matembezi ya amani ya waumini wa Kiislamu waliokuwa wakishiriki maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) katika mji mkuu Abuja.