Sep 04, 2023 07:51 UTC
  • Mwakilishi wa Sheikh Zakzaky:  Ayatullah Khamenei ameifundisha dunia muqawama na kusimama kidete

Mwakilishi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameifundisha dunia nzima muqawama na kusimama kidete.

Sheikh Adam Soho Ahmad amesema hayo akiwa Karbala Iraq kwa ajili ya kushiriki Arubaini ya Imam Hussein ambapo sambamba na kubainisha kwamba, Ayatullah Khamenei ni kiongozi wa harakati ya muqawama ameeleza kwamba, muqawama na mapambano ni tumaini pekee la watu huru duniani kwa ajili ya kukabiliana na mabeberu wa dunia.

Mwakilishi huyo wa Sheikh Ibrahim Zakzaky ameongeza kuwa, Ayatullah Khamenei kama alivyokuwa Imam Ruhullah Khomeini, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anawafundisha walimwengu wote na Sheikh Ibrahim Zakzaky amejifunza muqawama na kusimama kidete kutoka kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria

 

Sheikh Adam Soho Ahmed amebainisgha pia kuwa, Arubaini ya Imam Hussein (as) ni nembo ya mshikamano na mfunagamno wa watu huru duniani na kwamba, hii leo wameshikamana bega kwa bega kwa ajili ya kuleta hamasa ya kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (as).

Kadhalika amesema kuwa, tunapaswa kumshukuru Imam Hussein (as) ambaye amewaleta pamoja watu wote wa dunia hii leo, na kuongeza kuwa Imamu Hossein (as) alisimama kuamrisha mema na kukataza maovu na hiii leo kuunga mkono harakati ya muqawama ni mfano wa wazi wa kuamrisha mema.

Tags