Aug 14, 2025 02:32 UTC
  • Leo Katika Historia
    Leo Katika Historia

Leo ni Alkhamisi tarehe 20 Safar 1447 Hijria sawa na tarehe 14 Agosti 2025.

Siku kama ya leo miaka 1386 iliyopita, ilifanyika majlisi ya kwanza ya siku ya Arubaini tangu kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein bin Ali (as) na watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume ambao waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria.

Majlisi ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume na masahaba zake watiifu ambao walisabilia roho zao katika ardhi ya Karbala kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu.   

Siku kama ya leo miaka 133 iliyopita, alizaliwa Ayatullah al-Udhma Mar’ashi Najafi mmoja wa maulama wakubwa wa Kiislamu katika mji wa Najaf nchini Iraq.

Baba yake ni Sayyid Shamsuddin Mahmoud Mar’ashi aliyekuwa miongoni mwa wanazuoni na mafaqihi wakubwa katika zama zake. Baada ya kukamilisha masomo ya awali na ya Kiislamu huko Najaf, Mar’ashi Najafi alianza kuhudhuria darsa na masomo ya Usul kwa Agha Dhiyau Iraqi na Sheikh Ahmad Kashif al-Ghitaa.

Ayatullah Mar’ashi Najafi alipata daraja ya juu ya elimu yya Ij’tihad akiwa na umri wa miaka 27.

Ayatullah Sayyid Mar’ashi Najafi

Siku kama ya leo miaka 187 iliyopita, hatimaye baada ya miaka 15 ya mapambano dhidi ya wavamizi Wafaransa nchini Algeria, Amir Abdul-Qadir al-Jazairi alitiwa mbaroni na wavamizi hao.

Sababu ya kushindwa Abdul-Qadir ni kuwa, mwanamapambano huyo hakuwa na kambi na vituo vya kuendeshea harakati ndani ya Algeria. Maeneo yote ya nchi hiyo yalikuwa chini ya udhibiti wa wavamizi Wafaransa. Ndio maana alilazimika kuendesha harakari na mapambano yake katika maeneo ya mpakani baina ya Algeria na Morocco. 

Amir Abdul-Qadir al-Jazairi alifungwa jela kwa miaka 9 nchini Ufarasa na baadayae akaachiliwa huru kwa sharti kwamba asirejee nchini Algeria.  ***

Tarehe 14 Agosti miaka 79 iliyopita yaani tarehe 14 Agosti mwaka 1945 Japan ilisalimu amri mbele ya vikosi vya Waitifaki.

Kwa utaratibu huo vita vilivyokuwa vimeanza mwaka 1939 kwa mashambulizi ya Ujerumani dhidi ya Poland vikafikia kikomo. Japan na Marekani ziliingia katika vita vikali Disemba mwaka 1941.

Vita hivyo vilimalizika baada ya Marekani kushambulia miji ya Hiroshima na Nagasaki kwa mabomu ya nyuklia ambayo yaliua karibu watu laki mbili. Kusalimu amri huko kwa Japan kwa hakika kulihitimisha Vita vya Pili vya Dunia. 

Siku kama ya leo miaka 78 iliyopita, nchi ya Pakistan ilijitenga rasmi na India na kujitangazia uhuru wake.

Dini tukufu ya Kiislamu iliingia Bara Hindi katika karne ya 8 na sehemu ya ardhi hiyo ambayo leo inajulikana kwa jina la Pakistan ilikuwa mikononi mwa Waislamu hadi wakati ilipokaliwa kwa mabavu na Waingereza mwishoni mwa karne ya 18.

Chama cha Muslim League kikiongozwa na Muhammad Ali Jennah kilianzishwa mwaka 1906 kwa lengo la kuunda serikali ya Kiislamu baada ya kuanza harakati za wananchi wa India dhidi ya mkoloni Mwingereza. Chama hicho kilifanikiwa kuwashawishi Waislamu wa India na hatimaye kiliunda nchi ya Pakistan.

Katika siku kama ya leo miaka miaka 69 iliyopita yaani tarehe 14 Agosti 1956, aliaga dunia malenga na mwandishi wa Kijerumani aliyejulikana kwa jina la Bertolt Brecht.

Brecht alizaliwa mwaka 1898 Miladia katika jimbo la Ugsbourg nchini Ujerumani. Malenga na mwandishi huyo wa Kijerumani alihitimu elimu ya juu katika taaluma ya sayansi asilia (bayolojia, kemia na fikikia). Malenga huyo wa Kijerumani ameacha vitabu na picha ambazo nyingi zinaeleza kuhusu utawala wa Manazi na udhalimu waliokuwa wakiutenda. 

Na siku kama ya leo miaka 19 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 14 Agosti 2006, yalimalizika mapigano kati ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon na utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya kutolewa azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilikubaliwa na pande hizo mbili. Mapigano hayo yaliyoanzishwa na utawala haramu wa Israel tarehe 12 Juni 2006, yalikuwa na lengo la kuidhoofisha na hata kuisambaratisha harakati ya Hizbullah. Kusimama kidete kwa wapiganaji wa Hizbullah dhidi ya majeshi ya Israel, kulimfanya Katibu Mkuu wake Sayyid Hassan Nasrullah apate uungaji mkono mkubwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Baada ya kukabiliwa na mapambano makali ya wapiganaji shupavu wa Hizbullah askari wa Kizayuni ambao awali walikataa mpango wa kusitisha vita walilazimika kuukubali mpango huo na kurudi nyuma bila ya mafanikio yoyote.   ****