Sep 22, 2021 12:44
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambaye ni mwenyekiti sasa wa Umoja wa Afrika AU amewasilisha malalamiko kadhaa ya bara hilo katika mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ulioanza jana mjini New York, likiwemo la bara la Afrika kupatiwa uanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN.