-
Magaidi Madaesh 87 wahojiwa Iraq ili kupata fununu kuhusu Abubakar Al-Baghdadi
Jul 26, 2017 03:08Wizara ya Ulinzi ya Iraq imetangaza kuwa magaidi 87 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, raia wa nchi 17 tofauti wanasailiwa kwenye jela za usalama za nchi hiyo ili kupata fununu na taarifa kuhusu kinara wa kundi hilo la kitakfiri Abubakar Al-Baghdadi.
-
Mamia ya maiti za wanachama wa Daesh (ISIS) zimerundikana Libya
Jul 24, 2017 03:47Serikali ya Libya imesema mamia ya maiti za wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) raia wa kigeni zimerundikana nchini humo, miezi kadhaa baada ya wapiganaji hao kushindwa na vikosi vya serikali katika mji wa Pwani wa nchi hiyo wa Sirte.
-
Shirika la Ujasusi la Ujerumani: Mamia ya raia wa nchi hiyo ni wanachama wa Daesh
Jul 23, 2017 13:54Shirika la Ujasusi la Ujerumani limesema kuwa raia wa nchi hiyo 930 ni wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh.
-
Syria yaitaka Marekani na washirika wake walipe fidia ya uharibifu
Jul 23, 2017 02:49Serikali ya Syria imeliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiitaka Marekani na muungano wake usio halali kuilipa fidia serikali ya Damascus kutokana na uharibifu unaotokana na mashambulizi ya muungano huo yanayolenga na kuharibu miundombinu ya nchi huyo.
-
Nouri al-Maliki: Iraq haitakuwa pamoja na nchi za Kiarabu dhidi ya Iran
Jul 22, 2017 02:29Nouri al-Maliki, Makamu wa Rais wa Iraq amesema kuwa, nchi yake haitakuwa pamoja na nchi za Kiarabu kwa ajili ya kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kubainisha kwamba, jambo hilo halitawezekana.
-
Jeshi la Iraq: Daesh wanawaua kwa umati watu wa familia za wapiganaji wake
Jul 18, 2017 15:26Duru za kiusalama nchini Iraq zimefichua kuwa, kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) limefanya mauaji ya umati dhidi ya watu wa familia za wanachama wake kufuatia fatwa iliyotolewa na mashekhe wa kundi hilo katika mji wa Tal Afar magharibi mwa mkoa wa Nainawa (Nineveh) nchini Iraq.
-
Jasusi mkubwa wa kike wa genge la Daesh ambaye pia ni kamanda, anaswa mjini Mosul
Jul 17, 2017 14:20Jeshi la Iraq limefanikiwa kumtia mbaroni jasusi mkubwa wa kike aliyekuwa akitumika na kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) mjini Mosul.
-
Al Abadi: Kukombolewa Mosul ni mwanzo wa kumalizika Daesh
Jul 17, 2017 07:22Waziri Mkuu wa Iraq amesema kuwa kushindwa magaidi katika mji wa Mosul kaskazini mwa nchi hiyo ni mwanzo wa kusambaratika kundi la kitakfiri la Daesh.
-
Iraq: Kiongozi wa Daesh, Abu Bakar al Baghdadi, bado yuko hai
Jul 16, 2017 15:12Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq imekanusha habari za kuuawa kiongozi wa kundi la kigaidi na la wakufurishaji la Daesh (ISIS) na kusema kuwa Abu Bakar al Baghdadi bado yuko hai na amejificha nchini Syria.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran asema ISIS haina uhusiano wowote na Uislamu
Jul 13, 2017 02:35Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema kundi la kigaidi la ISIS au Daesh halina uhusiano wowote na Uislamu na ni tishio kwa dunia nzima.