Syria yaitaka Marekani na washirika wake walipe fidia ya uharibifu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i32132-syria_yaitaka_marekani_na_washirika_wake_walipe_fidia_ya_uharibifu
Serikali ya Syria imeliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiitaka Marekani na muungano wake usio halali kuilipa fidia serikali ya Damascus kutokana na uharibifu unaotokana na mashambulizi ya muungano huo yanayolenga na kuharibu miundombinu ya nchi huyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 22, 2017 22:19 UTC
  • Syria yaitaka Marekani na washirika wake walipe fidia ya uharibifu

Serikali ya Syria imeliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiitaka Marekani na muungano wake usio halali kuilipa fidia serikali ya Damascus kutokana na uharibifu unaotokana na mashambulizi ya muungano huo yanayolenga na kuharibu miundombinu ya nchi huyo.

Damascus pia imetoa wito wa kukomesha mara moja mashambulizi hayo.

Syria imetoa matakwa hayo katika barua mbili zilizotumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Baraza la Usalama la umoja huo.

Serikali ya Damascus imesisitiza kuwa, mashambulizi hayo lazima yakomeshwe na kwamba, wanachama wa umoja huo usio halali lazima wawajibike kisiasa na kisheria kuhusu uharibifu wa miundombinu katika Jamhuri ya Kiarabu ya Syria, ikiwa ni pamoja na wajibu wa kulipa fidia za kuharibu miundombinu ya nchi hiyo.

Barua hiyo imesisitiza kuwa, mashambulizi ya Marekani na washirika wake yanaendelea kuua raia wasio na hatia kwa kisingizio cha kuwalenga wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh.

Uharibifu wa mashambulizi ya Marekani na waitifaki wake, Syria

Barua ya Syria kwa Umoja wa Mataifa la Baraza la Usalama imeashiria mashambulizi yaliyofanywa na ndege za muungano wa Marekani tarehe 27 May katika kijiji cha Hasu Albu Awf ambayo yaliharibu nyumba za raia wa eneo hilo la kuua raia wengi wakiwemo watoto wadogo.

Ijumaa ya jana Muungano huo wa Marekani na waitifaki wake ulitangaza kuwa, umeharibu taasisi na vituo kadhaa vya mafuta na gesi katika maeneo mbalimbali ya Syria ambavyo ulidai vilikuwa vikidhibitiwa na kundi la kigaidi la Daesh.

Vilevile Marekani na washirika wake wamekiri kuwa, mashambulizi za ndege zao yameua raia wasiopungua 603 huko Syria na Iraq japokuwa duru za kijitegemea sinasisitiza kuwa, idadi ya raia waliouawa na Marekani na washirika wake ni kubwa zaidi.