-
Ushirikiano na nchi za Mashariki ya Kati; stratijia ya Iran ya kulinda usalama wa safari za baharini Ghuba ya Uajemi
Sep 30, 2019 04:07Hossein Dehghani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika Masuala ya Sheria na Kimataifa amesema katika kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC pambizoni mwa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York Marekani kwamba, mizozo ya aina yoyote ni hatari kwa eneo hili zima.
-
Ukosoaji mkali wa Sergey Lavrov kuhusiana na miamala haribifu ya Marekani dhidi ya mapatano ya JCPO na Ghuba ya Uajemi
Sep 29, 2019 23:06Hatua zilizo kinyume cha sheria za Marekani kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA mwezi Mei mwaka jana na kisha kuiwekea Iran vikwazo vikali ambavyo vilikuwa havijawahi kushuhudiwa tena huko nyuma, na baada ya hapo kuzidisha uwepo wake wa kijeshi katika Ghuba ya Uajemi ambao umeshadidisha mizozo katika eneo hilo la kistratijia, ni mambo ambayo yameizidishia wasi wasi serikali ya Russia.
-
Zarif: Iwapo Marekani inataka mazungumzo na Iran lazima itekeleze ahadi zake
Sep 29, 2019 03:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran haitaacha mustakabali wa uchumi na wananchi wake utegemee mkutano wa kimaonyesho na Rais Donald Trump wa Marekani. Ameongeza kuwa, kama ambavyo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alivyosema, 'iwapo Mareknai inataka kufanya mazungumzo na Iran, ni lazima kwanza itekeleze ahadi zake na isitishe vikwazo.'
-
Katika mtazamo wa Kansela wa Ujerumani; Mwarubaini wa kupunguza mivutano Magharibi ya Asia ni kurejea kwenye JCPOA
Sep 18, 2019 07:25Kwa mtazamo wa Umoja wa Ulaya na Troika ya umoja huo inayoundwa na Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yana mchango muhimu sana katika kulinda amani na usalama katika eneo la Magharibi ya Asia na katika uga wa kimataifa. Kwa mtazamo wa nchi za Ulaya, kujitoa Marekani katika JCPOA kumekuwa chanzo cha kujitokeza mivutano na hali ya wasiwasi katika Ghuba ya Uajemi na Magharibi ya Asia.
-
Baqeri: Iran iko tayari kulinda kikamilifu maslahi yake katika Ghuba ya Uajemi
Sep 12, 2019 06:56Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kulinda kikamilifu usalama na maslahi yake katika Ghuba ya Uajemi."
-
Ukosoaji wa Russia kwa nafasi haribifu ya Magharibi katika Ghuba ya Uajemi
Sep 10, 2019 22:01Baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutangaza kuiondoa nchi hiyo katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia mashuhuri kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) mnamo tarehe 8 Mei mwaka uliopita, alianza kutekeleza mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Iran.
-
Sisitizo la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa EU juu ya kulinda makubaliano ya JCPOA na kuimarisha usalama wa Ghuba ya Uajemi
Aug 31, 2019 07:40Umoja wa Ulaya pamoja na Troika ya Ulaya zikiwa wanachama wa kundi la 4+1 mara kadhaa zimesisitiza kuwa kuna udharura wa kuyalinda makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na wakati huo huo kurejesha uthabiti na usalama katika Ghuba ya Uajemi kwa kuzingatia chokochoko za Marekani katika eneo hilo la maji lenye umuhimu wa kijio-stratejia.
-
Salami: Usalama Ghuba ya Uajemi utapatikana kwa ushiriki wa Iran
Aug 24, 2019 03:02Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: "Usalama katika Ghuba ya Uajemi utapatikana kwa uwepo wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Zarif: Marekani haina uwezo wa kuvuruga usalama wa Ghuba ya Uajemi
Aug 22, 2019 22:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inafanya juhudi zake zote kulinda usalama wa Ghuba ya Uajemi na kwamba Marekani haina uwezo wa kuvuruga usalama wa eneo hilo.
-
Admeri Tangsiri: Hatutakubali kabisa Marekani na Uingereza ziwepo katika Ghuba ya Uajemi
Aug 20, 2019 03:34Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inazitangazia nchi za eneo na ulimwengu mzima kwamba, haitakubali kabisa uwepo wa Marekani, Uingereza na nchi nyingine yoyote ile itakayotaka kuzusha moto katika eneo la Ghuba ya Uajemi.