Admeri Tangsiri: Hatutakubali kabisa Marekani na Uingereza ziwepo katika Ghuba ya Uajemi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55490-admeri_tangsiri_hatutakubali_kabisa_marekani_na_uingereza_ziwepo_katika_ghuba_ya_uajemi
Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inazitangazia nchi za eneo na ulimwengu mzima kwamba, haitakubali kabisa uwepo wa Marekani, Uingereza na nchi nyingine yoyote ile itakayotaka kuzusha moto katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 20, 2019 03:34 UTC
  • Admeri Tangsiri: Hatutakubali kabisa Marekani na Uingereza ziwepo katika Ghuba ya Uajemi

Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inazitangazia nchi za eneo na ulimwengu mzima kwamba, haitakubali kabisa uwepo wa Marekani, Uingereza na nchi nyingine yoyote ile itakayotaka kuzusha moto katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Admeri Alireza Tangsiri amesema, kupita kwenye Lango Bahari la Hormuz ni huru kwa wote; na Iran inadhamini usalama wa suala hilo. Lakini amesisitiza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itasimama imara kukabiliana na nchi za nje ya eneo hili na maajinabi ambao wanajiingiza kwenye Ghuba ya Uajemi kwa madhumuni ya kutoa vitisho, kuvuruga amani na kuzusha machafuko; na itatekeleza jukumu lake la kuhakikisha amani inakuwepo katika eneo hilo.

Boti ya IRGC ikifanya doria katika maji ya Ghuba ya Uajemi

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la SEPAH aidha ameeleza bayana kuwa: Nchi za eneo zitambue kuwa, Iran inayanyooshea mkono wa udugu na urafiki mataifa na nchi za Kiislamu; na muungano uliobuniwa wa kusindikiza vyombo vya majini hautaweza kuyumbisha utekelezaji majukumu wa IRGC, ambao ni kulinda na kudhamini amani na usalama katika eneo hili.../