-
Makundi ya muqawama yasisitiza kuunganisha juhudi ili kukabiliana na mashambulizi ya Israel
Mar 20, 2025 07:00Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) zimesisitiza juu ya haja ya kuunganisha juhudi makundi ya muqawama ya Palestina na nchi za Kiarabu ili kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kuunga mkono mapambano ya ukombozi katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza na kupinga mipango ya Marekani na utawala wa Kizayuni ya kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina.
-
Moto mpya wa vita wawashwa na utawala wa Kizayuni huko Gaza kwa msaada wa Marekani
Mar 20, 2025 06:22Kwa kukiuka makubaliano ya usitishaji vita huko Ghaza yaliyoanza kutekelezwa tarehe 19 Januari, utawala wa Kizayuni umeanzisha tena vita vya umwagaji damu dhidi ya eneo hilo lililoharibiwa na vita, kwa kufanya mashambulizi makubwa ya kinyama ambayo yamesababisha mauaji ya mamia ya mashahidi wa Kipalestina na kujeruhi wengine wengi katika ukanda huo.
-
Hamas: Marekani ni mshirika wa moja kwa moja katika vita dhidi ya watu wa Gaza
Mar 19, 2025 04:11Msemaji wa harakati ya Hamas amesema harakati hiyo inatekeleza kikamilifu masharti ya makubaliano ya usitishaji vita na kwamba Wazayuni wameyakiuka akisisitiza kuwa, uratibu wa awali wa utawala huo ghasibu na Washington wa kuanzisha tena vita dhidi ya watu wa Gaza unaashiria ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani katika jinai zinazofanywa Wazayuni.
-
Maafisa 5 waandamizi wa HAMAS wauawa shahidi katika mashambulio ya Israel Ghaza
Mar 19, 2025 00:44Maafisa watano waandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wameuawa shahidi kufuatia mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.
-
Hamas yalaani ya mashambulizi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen
Mar 16, 2025 23:07Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani vikali mashambulizi ya anga ya Marekani na Uingereza dhidi ya maeneo ya makazi ya watu huko Sana'a, mji mkuu wa Yemen.
-
Hamas: Oparesheni ya Salfit ni ujumbe wa muqawama katika kujibu chokochoko za adui
Mar 13, 2025 04:03Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesisitiza katika taarifa kuwa oparesheni ya ufyatuaji risasi iliyotekelezwa jana usiku karibu na eneo la Salfit katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni jibu jipya la watu wao na wanamuqawama huru wa Palestina katika kujibu mashambulizi ya kikatili ya utawala ghasibu wa Israel khususan kaskazini mwa ukingo huo.
-
Hamas: Duru mpya ya mazungumzo ya kusitisha mapigano imeanza
Mar 12, 2025 22:52Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameeleza kuwa duru mpya ya mazungumzo ya kusimamisha vita Ukanda wa Gaza, imeanza.
-
Hamas: Taifa la Palestina litajitawala lenyewe katika ardhi yake
Mar 11, 2025 03:32Mmoja wa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema: "Gaza" na "Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni mali ya wenyeji wa maeneo hayo.
-
HAMAS yasema imejiandaa 'kwa chochote kitachotokea' baada ya 'onyo la mwisho' alilotoa Trump
Mar 07, 2025 00:02Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS zimetangaza kwamba, zimejiandaa kwa "chochote kitachotokea" na zingali ziko kwenye hali ya "tahadhari kamili", zikisisitiza kuwa, vitisho vya utawala wa Kizayuni wa Israel vya kuanzisha tena vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza havitatoa hakikisho kwa utawala huo dhalimu la kuweza kuwakomboa mateka wake.
-
White House yakiri: US imefanya mazungumzo ya moja kwa moja na HAMAS
Mar 06, 2025 23:02Ikulu ya White House imethibitisha ripoti inayodai kuwa Marekani imefanya mazungumzo ya moja kwa moja na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas, yenye makao yake katika Ukanda wa Gaza.