-
Seneta wa Marekani ataka uchunguzi kuhusu kuuliwa kigaidi viongozi wa Yemen
Oct 23, 2018 03:24Bi Elizabeth Warren, mjumbe katika Baraza la Senate la Marekani ameiandikia barua wizara ya mahakama ya nchi hiyo na kutaka kufanyike uchunguzi kuhusu ripoti zinazosema kwamba, maveterani wa kivita na wanajeshi wastaafu wa Marekani wanatumiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kuua kigaidi viongozi wa kisiasa wa Yemen.
-
'Saudia na Imarati zimehusika na shambulio la kigaidi la Ahvaz nchini Iran'
Sep 23, 2018 10:41Katibu wa Baraza la Kitaifa la Wairani wa Marekani linalojulikana kwa jina la NIAC amesema kuwa, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zimehusika katika shambulizi la kigaidi lililotokea jana Jumamosi katika makao makuu ya mkoa wa Khuzistan wa kusini magharibi mwa Iran.
-
Imarati yaondoa kikosi cha mwisho cha askari wake Yemen
Sep 23, 2018 04:22Kikosi cha mwisho cha wanajeshi wa Umoja wa Falme za Kiarabu kilichokuwa kikihudumu chini ya muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika mkoa wa Mahran nchini Yemen kimewasili nyumbani baada ya serikali ya Abu Dhabi kukiagizi kiondoke katika nchi hiyo maskini ya Kiarabu.
-
Seif al Islam Gaddafi akutana na viongozi wa ngazi za juu wa Imarati na Misri
Sep 17, 2018 10:57Baadhi ya duru za ngazi za juu za Libya na Misri zimetangaza kuwa, Seif al Islam, mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, amekutana na viongozi wawili wakubwa wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri.
-
Vipigo vya makombora ya Yemen dhidi ya mishipa ya kiuchumi ya Saudia na Imarati
Sep 05, 2018 01:40Jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen zimeamua kulipiza kisasi cha jinai zinazofanywa na Saudi Arabia na wavamizi wenzake, kupitia kushambulia kwa makombora mishipa ya kiuchumi ya Saudia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
-
UAE ilitumia spyware ya Israel kuwafanyia ujasusi viongozi wa eneo
Sep 01, 2018 09:33Utawala wa Umoja wa Falme za Kiarabu ulitumia programu ya kijasusi ya kudukua kompyuta au simu za mkononi (spyware) kuwafanyia ujasusi viongozi kadhaa wa nchi za Kiarabu akiwemo Amir wa Qatar, Waziri Mkuu wa Lebanon na mwanamfalme mmoja wa Saudia.
-
Ufaransa yadai kuwa wavamizi hawatumii silaha zake katika jinai zao Yemen
Sep 01, 2018 02:56Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa amedai kuwa, silaha za Ufaransa zilizouziwa Saudia na Imarati sizo zinazotumika kufanya mauaji ya raia nchini Yemen.
-
Qatar yaonyesha wasi wasi wake kutokana na ujasusi unaofanywa na Imarati dhidi yake
Sep 01, 2018 00:08Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetoa taarifa ikionyesha wasi wasi wake juu ya ujasusi unaofanywa na baadhi ya shakhsia wa Imarati dhidi ya nchi hiyo.
-
Saudia na Imarati zinailaghai Jordan iunge mkono mpango wa Marekani wa Muamala wa Karne
Aug 31, 2018 23:38Mbunge wa Jordan, Khalid Ramadhan amefichua hila na ulaghai mpya unaofanywa na Saudi Arabia ikishirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu, Imarati wa kuishawishi Jordan iunge mkono mpango wa Marekani wa kuiangamiza Palestina unaojulikana kama "Muamala wa Karne".
-
Qatar yazishutumu Saudia, UAE kwa kushirikiana na magaidi wa al Qaeda nchini Yemen
Aug 31, 2018 02:02Balozi wa Qatar nchini Marekani amezishutumu Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kuwa na ushirikiano wa siri na magaidi wa al-Qaeda nchini Yemen.