Seneta wa Marekani ataka uchunguzi kuhusu kuuliwa kigaidi viongozi wa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i48983-seneta_wa_marekani_ataka_uchunguzi_kuhusu_kuuliwa_kigaidi_viongozi_wa_yemen
Bi Elizabeth Warren, mjumbe katika Baraza la Senate la Marekani ameiandikia barua wizara ya mahakama ya nchi hiyo na kutaka kufanyike uchunguzi kuhusu ripoti zinazosema kwamba, maveterani wa kivita na wanajeshi wastaafu wa Marekani wanatumiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kuua kigaidi viongozi wa kisiasa wa Yemen.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Oct 23, 2018 03:24 UTC
  • Seneta wa Marekani ataka uchunguzi kuhusu kuuliwa kigaidi viongozi wa Yemen

Bi Elizabeth Warren, mjumbe katika Baraza la Senate la Marekani ameiandikia barua wizara ya mahakama ya nchi hiyo na kutaka kufanyike uchunguzi kuhusu ripoti zinazosema kwamba, maveterani wa kivita na wanajeshi wastaafu wa Marekani wanatumiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) kuua kigaidi viongozi wa kisiasa wa Yemen.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mapema leo asubuhi, Bi Warren amesema katika barua yake hiyo ya tarehe 19 Oktoba kwamba kuna haja ya kupewa adhabu viongozi na maafisa wa Marekani ambao watabainika wameshiriki kwa namna yoyote ile katika kuwaua viongozi wa kisiasa wa Yemen au hata kama walikuwa na taarifa na jambo hilo na wasichukue hatua.

Tarehe 17 mwezi huu wa Oktoba, mtandao wa BuzzFeed ulifichua siri inayoonesha kuwa, maafisa wastaafu wa jeshi la Marekani wameshirikiana na shirika moja lenye mfungamano na Umoja wa Falme za Kiarabu yaani Imarati kuua wapinzani wa kisiasa wa Abu Dhabi katika mji wa Aden wa kusini mwa Yemen.

Jela ya siri ya Imarati mjini Aden, kusini mwa Yemen

 

Mwezi Machi 2015, Saudi Arabia kwa uungaji mkono wa Marekani, Israel, Imarati na nchi nyingine kadhaa, ilianzisha mashambulizi ya pande zote ya kijeshi dhidi ya nchi maskini ya Kiarabu ya Yemen baada ya kuizingira kila upande kutokea, ardhini, bahari na angani.

Hadi hivi sasa vita hivyo vya kivamizi vya Saudia na kundi lake dhidi ya nchi ya Waislamu ya Yemen vimeshaua zaidi ya Wayemen elfu nne, kujeruhi makumi ya wengine na kuwafanya wakimbizi mamilioni ya raia wa nchi hiyo.

Uvamizi huo umeisababishia nchi maskini ya Yemen matatizo mengi yakiwemo ya upungufu mkubwa wa chakula  na madawa.